Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili katika ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo jengo la TTCL mtaa wa Samora leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa mifumo na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika uendeshaji wa shughuli za serikali. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea taarifa kuhusu maendeleo ya Tovuti Kuu mpya ya serikali inayosimamiwa na Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma. Balozi Sefue amefafanua kuwa Tovuti Kuu ya Serikali iliyoanzishwa itawawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali. Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa serikali katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika shughuli za serikali kupitia Tovuti Kuu mpya ya serikali iliyoanzishwa kwa lengo la kuboresha na kurahisisha utoaji wa taarifa na huduma kwa umma, kuhamasisha ushirikishwaji wa raia katika utoaji wa maamuzi yanayowahusu na kuwezesha uwepo wa serikali iliyo wazi.
Baadhi ya viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao iliyo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Picha na 5. Mwonekano mpya wa Tovuti Kuu ya Serikali ambayo inapatikana katika anuani ya www.egov.go.tz.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
……………………………………………………………………………….
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
SERIKALI YASEMA TEHAMA KUFIKA HADI VIJIJINI
SERIKALI imesema kwamba inatarajia kuboresha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kila kijiji ili huduma zake ziweze kuwa karibu na wananchi, hatua hiyo itasaidia kuwapunguzia gharama wanazozitumia.
Aidha Serikali imeeleza kwamba iteendelea kujenga uwezo wa kiufundi wa kuweza kuzuia uvujaji wa siri, uhalifu na udhibiti wa sheria ndani ya vyombo vyake ili taarifa za siri zisiweze kuvuja.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Serikali Mtandao(e GA) jijini Dares Salaam kwa ajili ya kuzungumza na menejimenti na wafanyakazi.
“Leo nimetembelea ofisi hii. Ni eneo la kipaumbele kwa Serikali kwa kuongeza matumizi ya TEHAMA kwa Serikali, tija, kasi ya utendaji kazi na huduma za Serikali. Hivyo sehemu hii ni muhimu ya kuifanya Serikali iwe karibu na wananchi. Tovuti hii iwe ni dirisha la mwananchi kutatuliwa shida yake.,”alisema huku akitoa wito kwa wananchi wawe tayari kuitumia.
Balozi Sefue alisema tatizo la changamoto la TEHAMA kuhusu uvujaji wa siri lipo dunia nzima hata Marekani wanakabiliana nalo ,hivyo ufumbuzi wake si kuachana nalo bali kuzuia uvujaji huo na uhalifu kwa kujenga uwezo wa udhibiti.
“Lazima kuwe na udhibiti mfano wa kisheria tayari tunayo sheria tutaendelea kuiboresha kulingana na changamaoto zitakazo kuja,” alisisitiza Balozi Sefue.
Alisema kupitia TEHAMA wananchi wataweza kupata matibabu au elimu na kulizia huduma wanazotakiwa kuzipta mfano miradi ya visima vya maji imefikia hatua zipi.
Aliongeza kuwa hivi sasa wakala huo unaandaa mifumo ya kuwezesha Wizara, Idara na taasisi mbalimbali za Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano.
Akizungumzia kuhusu ufikishaji wa huduma katika maeneo ya vijijini, Mtendaji Mkuu wa (eGA) Dk. Jabiri Bakari alisema watatumia ubunifu ili kuhakikisha huduma ya TEHAMA inatumika kwenye maeneo hayo mfano kwa kutumia sehemu za mkononi za kawaida.
Wakala hiyo ulianzishwa Julai mwaka 2012, ambapo taarifa mbalimbali za Serikali kutoka Wizara, Idara , wakala na taasisi zake zitapatikana kupitia mtandao wa wakala hiyo.
0 comments:
Post a Comment