Mhariri Mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu akizingumza na waandishi wa habari waliOpata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ya kuripoti habari za ukatili wa kijinsia yaliyotoleawa na Muungano wa waandishi wanawake Tanzania TAMWA jijini Mbeya Jana. (Picha na Furaha Eliab, Mbeya)Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandolo akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusiana na ukatili wa kijinsia yaliyotolewa na chama cha waandishi wanawake Tanzania (TAMWA).Masa Ngwila ambaye ni muwezeshaji wa semina kwa waandishi wa habari juu ya unyanyasaji wa kijinsia iliyotolewa kwa waandishi wa nyanda za juu kusini, Mbeya, Iringa , Njombe, Songea, Rukwa na Katavi.Picha ya pamoja na mgeni rasmi
…………………………
Na Furaha Eliab, Mbeya
IMEBAINIKA kuwa bado kuna ukatili mkubwa wa kijinsia katika familia za jamii ya kitanzania ambao unafanyika kimya kimya na hutokea ndani ya nyumba kati ya mume na mke.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa waandishi wa habari kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia ya siku nne kwa baadhi ya waandishi wa habari wa Nyanda za juu kusini yaliyotolewa na chama cha wanahabari wanawake Tanzania TAMWA.
Alisema kuwa asilimia kubwa ya familia za kitanzania kuna ukatili mbalimbali wa kijinsia ambao umekuwa ukitokea kimya kimya.
Aliutaja ukatili huo kuwa ni ukatili wa Kingono, ubakaji, kipigo na ulazimishwaji wa mapezi kati ya wanandoa ambao umekuwa ukifanyika kisirisiri katika familia.
Kandoro alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kufanya utafiti wa ukatili wa aina hiyo na kuuripoti kisha kuielinisha jamii juu ya ukatili wa aina hiyo ambao umekuwa ukinyanyasa mtu mmoja mmoja katika familia.
Alisema kuwa ukatili huo pia umekuwa ukitokana na mila na desturi zilizopo katika jamii nyingi za kitanzania na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.
Aliongeza kuwa katika utafiti uliofanywa na watu mbalimbali kuhusiana na ukatili wa kijinsia unaofanywa katika ngazi ya familia umebaini kuwa asilimia kubwa umekuwa katika mkoa wa Dodoma lwa asilimia 71, huku mkoa wenye ukatili kwa asilimia ndogo ni mkoa wa Tanga, asilimia 16.
Kufuatia uwingi wa asilimia kubwa ya ukatili huo Serikali imetengeneza mwongozo wa kisera na mwongozo wa kutoa huduma kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia hasa dhidi ya watoto.
Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni mhariri mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu alisema kuwa waandishi kama wataelimisha jamii juu ya ukatili huo wananchi watajinasua katika ukatili huo.
Alisema kuwa kuwapo kwa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kunakwamisha nchi kusonga mbele kimaendeleo na wanaotendewa ukatili ni wanawake kwa asilimia kubwa na wao ndio chachu ya maendeleo kwa taifa lolote duniani.
Kwayu alisema kuwa katika taifa ambalo hakuna ukatili wa kijinsia, taifa hilo limesonga sana katika maendeleo yake.
0 comments:
Post a Comment