Friday, October 4, 2013

D92A2030PWANI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesifu juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani katika suala zima la uwekezaji , akisema kuwa serikali iko tayari kuziunga mkono juhudi hizo ili kuhakikisha uchumi wan chi unaimarika.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Pwani ameyasema hayo mara baada ya kuzindua rasmi kiwanda cha Azam Cola kinachomilikiwa na kampuni ya Bakharesa kilichoko katika eneo la Mwandege wilayani Mkuranga  mkoani  Pwani.
Mara baada ya kuzunguka na kujionea uzalishaji ndani ya Kiwanda hicho Rais Kikwete amesema nia ya serikali ni kuona Tanzania inakuwa na viwanda vingi vitakavyochangia kutengeneza fursa za ajira na kuliweka taifa katika ramani ya mataifa ya kati kiviwanda.
Naye waziri wa viwanda na Biashara Dr. Abdala Kigoda amesema kwa hivi sasa mkoa wa Pwani kuna viwanda vingi ambavyo vyote vinatengeneza fursa mbalimbali.
Kwa upande wao kampuni ya Bakharesa wamemuomba Rais Kikwete kuwatatulia tatizo la umeme ambalo limekuwa sugu kutokana na kwamba wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwa umeme wa jenereta.
Rais Kikwete ameendelea na ziara yake mkoani humo ambayo itachukua siku sita katika kuangalia miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video