Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KOCHA wa timu ya Taifa ya England, maarufu kwa jina la`Simba Watatu`, Roy Hodgson amethibitisha kuwa macho yake tayari yamemtazama kinda wa Manchester United, Adnan Januzaj na anaweza kuichezea timu hiyo baadaye.
Nyota huyo mwenye umri wa 18, raia wa Ubelgiji alifanya kazi kubwa jana baada ya kuandika mabao mawili kimiani na kuifanya Man United itoke nyuma kipindi cha pili na kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Sunderland katika dimba la Stadium of Light.
Alipoulizwa kama Januzaj siku moja ataichezea England, Hodgson, aliyehojiwa na BBC1 wakati wa mechi hiyo ya siku alisema: `Ndiyo, kama atakubali uraia na kuwa zao la nyumbani atacheza`.
Mafanikio ya moto: Kinda la Manchester United, Adnan Januzaj alipiga mabao mawili mazuri jana dhidi ya Sunderland
Mbele ya TV: Roy Hodgson alitokea katika Tv jana na kukiri kuwa anatamani kuona Januzaj inaichezea England kwa siku za usoni
Amefichua siri: Bosi wa Manchester United, David Moyes amesema chama cha soka nchini England, FA kimekuwa na mawasiliano juu ya Januzaj kuichezea England
`Amekuwa na United kwa muda mrefu na kiukweli jambo hilo litajitaji majadiliano makubwa kabla ya kumtumia mchezaji`
`Hakuna shaka, ni kijana mwenye kipaji kikubwa na tumeangaza macho yetu kwake, lakini mambo mengi yatahitaji kujadiliwa`.
Kabla ya Hodgson kuzungumza na MOTD, Kocha wa United alifichua siri wakati wa mkutano wa baada ya mechi na waandishi wa habari huku akiwa ameibuka na ushindi.
Wakti Mbelgiji huyo akiwaniwa kimataifa, Januzaj amepinga suala hilo, akisema anataka kuichezea Albania. Lakini ndugu zake wanasema pia ana sifa za kuichezea Uturuki au Serbia.
Lakini kwa mujibu wa sheria za FIFA juu ya uraia, nyota huyo anaweza kuichezea England kama ameishi kwa miaka mitano baada ya miaka 18 ya sasa, na hii inamaanisha anaweza kuwa na sifa za kuichezea England mpaka februari 2018.
‘Anaweza kuchagua taifa la kuchezea,’ alisema Moyes baada ya mechi ya Sunderland.
Aliulizwa kuthibitisha kama tayari FA wameonesha nia kwa mchezaji huyo kuichezea England, moyes alisema: Ndiyo! wameonesha`.
Amemkubali sana: Beki wa United, Rio Ferdinandamesema Januzaj ana maisha mazuri ya soka siku za usoni
0 comments:
Post a Comment