Na Gladness Mushi, Arusha
IDADI
ya wabunge wanawake kwenye nchi wanachama wa mabunge ya nchi za kusini
mwa Afrika (SADC) imeongezeka ingawaje kwa Tanzania bado baadhi ya
wanawake wanahofu kubwa ya kushiriki katika chaguzi mbalimbali kutokana
na changamoto zilizopo kwenye jamii
Hayo
yameelezwa na Anna Makinda ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakati akiongea na vyombo vya habari mapema leo
kuhusiana na mkutano wa 34 wa jukwaa la Mabunge ya Nchi wanachama wa
jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika unaotarajiwa kufunguliwa na
Makamu wa Raisi dkt Gharib Bilali mapema jumapili ijayo.
Aidha
Makinda alisema kuwa kuongezeka kwa wabunge wanawake katika mabunge ya
SADC kunatokana na juhudi mablimbali ambazo zinafanywa na jumuiya hiyo
hali ambayo nayo imefanya mabadiliko makubwa sana kwenye baadhi ya nchi.
Alisema
kuwa pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya wabunge wanawake katika
jumuiya hiyo lakini kwa Tanzania bado baadhi ya wanawake wanauoga na
hofu ya kushiriki katika chaguzi kuu jambo ambalo wanatakiwa kulipinga.
“hapa
tunaona kuwa hii idadi ya wanawake ni kubwa katika jumuiya hii ya SADC
lakini kupitia ongezeko hili ni muhimu sana kwa wanawake wa Tanzania nao
wakahakikisha kuwa wanajitokeza kwenye chaguzi mbalimbali na kushiriki
kwani uwezo wa wao kuwa wabunge upo na wasiogoope wala kujiwekea udhaifu
wa changamoto”aliongeza Makinda
Wakati
huo huo alidai kuwa wanawake wa Tanzania hawapaswi kukatishana tamaa
wao kwa wao na badala yake wanatakiwa kupena moyo hasa pale wagombea
wanawake wanapokutana na changamoto kubwa ambazo wakati mwingine
zinasababisha baadhi yao kukimbia nafasi za uongozi
Awali
akiongelea mkutano huo wa 34 alisema kuwa Nchi ya Tanzania imepewa
nafasi ya kuwa mwenyeji mkuu wa mkutano huo ambao utaweza kuwashirikisha
viongozi wa Mabunge mbalimbali kutoka SADC na hivyo kupitia mkutano huo
wataweza lkujadili mambo mbalimbali
Makinda
alisema kuwa mkutano huo utaaangalia vitu muhimu kwa nchi wananchama
kama vile vigezo vya kusimamia na kutathimini mwenendo wa chaguzi za
nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
“Kauli
mbiu ya mkutano huu ni vigezo vya kuendesha na kutathimini chaguzi kwa
nchi za kusini mwa Afrika hivyo basi hapa tutaweza kuangalia na
kukagua hilo hivyo tutaweza kupata hata majibu ambayo yatasaidia nchi
zetu”aliongeza Makinda.
0 comments:
Post a Comment