Wednesday, October 16, 2013

Na Waitara Meng’anyi, Tarime

Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungulia mlangao nyakati za usiku.

Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi  namba sita alikolazwa akiuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake  aliyemtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.

“Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia, baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo  kwa kidole” alisema Ghati.

Wakati anamwonesha lilipo panga na kumpa kurunzi,  Ghati hakujuwa kuwa nini kinafuata, alifikiri kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda  sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama uko sawa halafu arudi kulala.

“ Alipoipata ile panga akaniambia leo atanitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa  panga ile akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa
kulia  ukakatika kama unavyoona” alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani  hospitali ya Wilaya Tarime.

Wakati anafanyiwa ukatili huo alipiga kelele lakini majirani hawakuwahi kufika  kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika
maeneo hayo.
“Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa” alieleza .

Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.
“ Nimeishi naye kwa miaka minne sasa na tuna watoto wawili na tulikuwa tunaishi vizuri, tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka, lingine ni  baada ya kuoa mke wa pili ambapo alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu” alisema Ghati.

 Ghati hataweza kurudiana na mume wake huyo  kwa kitendo alichomfanyia kwa vile amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu mumewe kifungo jela ili  ajifunze kutokana ukatili aliomfanyia.

” Naomba serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya kutembelea kwa kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha watoto wangu maana ni wadogo na mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula” alisema.
Wananchi walioshuhudia kitendo hicho walionesha kusikitishwa  na kukilaani kuwa kinaendelea kuharibu jina na sifa ya Wilaya ya Tarime .

“ Sikifurahii kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa hali ya juu kwa binadamu mwenzako  na hii inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku  kutuona  sisi  ni
wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa, mahakama imuhukumu huyu mtu  adhabu kubwa inayomstahili ili liwe fundisho kwa wengine” alisema Mwita Machera aliyekuwa  hostalini hapo.

Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu  na kuamuru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.

Hata hivyo siku moja baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu za wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa Mwita alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.

“ Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha si jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu  japo si wote” alisema Kamugisha kwa nija ya simu.
KWA HISANI YA DJ SEK

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video