Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Mtandao
Hakika
soka lina mambo yake, jana usiku mashabiki wengi walifurika kushuhudia
mechi kali ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la Dunia mwakani nchini
Brazil kwa ukanda wa Afrika baina ya timu ya Taifa ya Ghana `Black
Stars` dhidi ya timu bora ya Misri `Mafarao`.
Ilikuwa
mechi nzuri sana kwani wenyeji Ghana waliingia uwanjani wakionekana
wanahitaji ushindi mnono ambapo dakika zote 90 walionesha soka safi na
kuwadhibiti vizuri sana Misri ambao walikuwa tishio zaidi hasa wakati wa
makundi kwani hawakuwahi kupoteza mechi.
Ingekuwa
hivyo kwa timu yoyote kujiandaa na kushindani zaidi kama ingekutana na
waarabu hao wanaocheza soka la Uhakika, lakini jana walitota vibaya sana
mbele ya Ghana waliosheheni majembe yao muhimu na kulala kwa idadi
kubwa ya mabao 6-1.
Mshambuliaji Asamoah Gyan alifunga mabao mawili dakika ya tano na 52, wakati Wael Gomaa alijifunga dakika ya 21.
Mohamed
Aboutrika aliifungia bao pekee Misri kwa penalti dakika ya 41, kabla ya
Majeed Waris kuifungia Ghana dakika ya 44, Sulley Muntari akafunga kwa
penalti dakika ya 72 na mchezaji mpya wa Chelsea, Christian Atsu
akahitimisha karamu ya mabao ya Ghana dakika ya 87.
Hatari tupu: Asamoah Gyan aliifungia Ghana mabao mawili
Kikosi
cha kilikuwa; Ghana: Dauda, Inkoom, Akaminko, Sumaila, Opare, Essien,
Muntari/Badu dk83, K Asamoah, A Ayew/Atsu dk83, Waris, Gyan/Wakasu dk79.
Misri:
Ekrami/El Shenawy dk57, A Fathi, W Gomaa, Nagieb, Shedid/Shikibala
dk46, Ashour/Mehamadi dk40, Ghaly, El Neny, Aboutrika, W Soliman na M
Salah.
0 comments:
Post a Comment