Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MENEJA
wa zamani wa Manchester United manager, kibabu, Sir Alex Ferguson
amesema hajutii kustaafu mapema mwaka huu kuifundisha klabu hiyo na ana
furaha ya kumpatia mbinu za mafanikioa mrithi wake David Moyes.
Ferguson alibwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu akiwa kocha mwenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya soka la England.
Katika
miaka yake 27 aliyokaa Man United, Mscotish huyo alikuwa tajiri wa
kubeba makombe na kwa wakati wote alikuwa kivutio kwa mashabiki wa soka
wa England na duniani kote.
Alibeba
makombe 13 ya ligi kuu soka nchini England, matano ya FA, Manne ya ligi
na mawili ya ligi ya mabingwa baranI Ulaya, UEFA.

Muda mwafaka: Sir Alex Ferguson amesema hajutii kuondoka Manchester United
Bado Ferguson,ambaye amebakia kuwa mkurugenzi na balozi wa United, anatambua kuwa ulikuwa muda mwafaka kwake yeye kukaa pembeni.
‘Maamuzi
yangu yalikuwa sahihi, najua ilikuwa kitu cha msingi kwangu kuachia.
Najua nilishafanya kazi yangu; alisema mzee huyo wa miaka 71 wakati
akihojiana na Daily Telegraph.
‘”Nitakumbuka
hili?” Akili yangu ilikuwa “Sitaweza kuacha kazi hii. Muda wangu
ulifika. Mafanikio yalikuwa makubwa, kufikiria yaliyotokea kipindi
changu haitakiwi. Sahau yaliopita. Hayana maana kwangu”

Njia
moja: Ferguson alikuwa katika sherehe za kubadilisha jina la barabara
na kuitwa `Barabara ya Sir Alex Ferguson` yaani ‘Sir Alex Ferguson Way’

Wasiwasi tupu: Haujakuwa mwanzo mzuri kwa kocha David Moyes aliyerithi mikoba ya Ferguson

Tabasamu
kubwa: Mscotish huyo hakuonekana kuwa na msongo wa mawazo wakati wa
mazoezi akiwa na Robin van Persie kujiandaa na mchezo dhidi ya
Southampton jumamosi hii
0 comments:
Post a Comment