Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
TIMU
ya Taifa ya England maarufu kwa jina la `Simba watatu` wamejihakikishia
nafasi ya kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani nchini Brazil baada
ya kuilaza Poland mabao 2-0.
Mabao hayo yalifungwa na Wayne Rooney na Nahodha Steven Gerrard ambapo mchezo huo ulipigwa katika Uwanja wa Wembley.
Kikosi cha Roy Hodgson jana kimewapa raha Waingereza kwa ushindi huo na sasa ni furaha nchi nzima England.
Mshambuliaji wa Manchester United, Rooney alianza kufunga dakika ya 41 na kiungo wa Liverpool, Gerrard akafunga dakika ya 88.
Kikosi
cha England kilikuwa: Hart, Smalling, Cahill, Jagielka, Baines,
Gerrard, Carrick/Lampard dk71, Townsend/Milner dk86, Rooney, Welbeck na
Sturridge/Wilshere dk82.
Poland:
Szczesny, Wojtkowiak, Jedrzejczyk, Glik, Celeban, Blaszczykowski,
Mierzejewski/Zielinski dk75, Krychowiak, Sobota/Pezsko dk65, M
Lewandowski/Klich dk46 na R Lewandowski..
Akipiga bao safi: Wayne Rooney akipiga kichwa na kukwamisha bao kimiani
Anapaa: Rooney (katikati) akishangilia bao lake na kuifanya England iongoze
Kazi ya pamoja: Wachezaji wa Englandwakishangilia na kumpongeza Rooney baada ya kufunga bao lake muhimu jana
Anabusu jezi: Rooney akionesha mapenzi yake kwa timu yake ya taifa baada ya kufunga bao la kwanza
0 comments:
Post a Comment