
CHAMA
Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimetuma salamu za
rambirambi kutokana na kifo cha Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu na
Usuluhishi, Jimmy Mhango aliyefariki juzi katika hospitali ya Muhimbili
jijini Dar es Salaam kutokana na presha.
Katibu
Mkuu wa DRFA Msanifu Kondo amesema leo (Oktoba 22) kwamba wamepokea kwa
masikitiko taarifa za kifo cha Mjumbe huyo, ambaye pia aliwahi kuwa
mchezaji mahiri katika timu ya Ushirika ya Moshi katika miaka ya tisini
chini ya Kocha Dan Korosso.
Marehemu pia aliwahi kuzichezea timu za Pan Africans ya Dar es Salaa pamoja na timu ya Mkoa wa Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Stars.
“DRFA
imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Jimmy Mhango na inatoa pole
kwa familia, ndugu jamaa na wanafamilia wote wa mpira wa miguu,
tunawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu,” alisema.
Kamati
ya Nidhamu na Usuluhishi ya DRFA ambayo marehemu alikuwa mjumbe,
inaongozwa na Roman Masumbuko (Mwenyekiti), Fahadi Kayuga (Makamu
Mwenyekiti), Mohamed Mpili (Mjumbe) na Peter Nkwera (Mjumbe).
Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo (Jumanne)katika makaburi ya Ilala Mchikichini, Dar es Salaam saa kumi jioni.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema
Imetolewa na Mohamed Mharizo
Ofisa Habari
Chama Cha Mpira Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
Oktoba 22, 201
0 comments:
Post a Comment