![]() |
Kocha wa Coastal Union, Hemed Morroco (wa kwanza kulia) hajafukuzwa na wagosi wa Kaya bali mkataba wake umekwisha |
Na Oscar Assenga, Tanga.
MJUMBE
wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Albert
Clement Peter “Mkubwa wa Kazi amekanusha vikali taarifa zilizosambazwa
na baadhi vyombo vya habari kuwa wamemfukuza kocha wao mkuu Hemed
Morroco.
Akizungumza
jana, Peter alisema wao hawajamfukuza kocha huyo kama ilivyoripotiwa
bali mkataba wake wa kuendelea kuinoa timu hiyo umekwisha hivyo
wataangalia hatima yake kama watamuongezea au la.
Alisema
hivi sasa kocha huyo yupo mjini Bukoba akiwa na kikosi cha timu hiyo
wakijiandaa na mechi yao dhidi ya Kagera Sugar ambayo itachezwa Jumamosi
hii kwenye dimba la soka la Kaitaba.
“Mimi
nashangaa sana kusikia baadhi ya vyombo vikiripoti tumemfukuza Morroco
hizo habari wamezitoa wapi jamani acheni uzushi Morroco bado ni kocha
wetu na yupo na timu bukoba “Alisema Peter.
Mjumbe
huyo alisema uongozi wa klabu hiyo umeshapitisha jina la msemaji wao na
hivyo wanatarajia kumtangaza muda wowote ambaye atachukua nafasi ya Edo
Kumwembe.
Alisema
mkataba wa kocha huyo uliisha tokea mwanzoni mwa mwezi huu ambapo bado
uongozi haujakaa naye na kuzungumza kuhusiana na mkataba mpya.
0 comments:
Post a Comment