Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Uruguay, Edinson Cavani amesema nyota mwenzake, Luis Suarez alikuwa anataka kwenda Real Madridi na hakupenda sana kujiunga na Arsenal.
Suarez alirudi kuitumikia Liverpool wikiendi iliyopita na kufunga mawili dhidi ya Sunderland na ulikuwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu nchini England tangu afungiwe mechi 10 kwa kitendo cha kumuuma beki wa Chelseai Branislav Ivanovic .
Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay alihusishwa na dili la kuondoka Anfield majira ya kiangazi mwaka huu na Arsenal walitoa dau la pauni milioni 41, lakini majogoo wa jiji walikataa kumuuza.

Na sasa Cavani ambaye alitengeneza pesa kubwa baada ya kuhama kutoka Napoli na kujiunga na Paris Saint-Germain – amesema bado Suarez ana ndoto ya kuhamia Real Madrid.
Cavani alisema: `Ni ajabu kwangu kuwa Luis amerudi Liverpool na kufunga mabao sahihi na kiufundi`.
`Ni mshambuliaji aliyekamilika zaidi nchini England- na ni mshambuliaji aliyekamilika duniani. Uwezo wake na kujiamini si tatizo kwake, atafunga mabao mengi msimu huu, nina uhakika`.


0 comments:
Post a Comment