Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KIUNGO
Michael Carrick anatarajiwa kupewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha
timu ya Taifa ya England kwenye mchezo muhimu mno kuwania kufuzu fainali
za kombe la Dunia mwakani nchini Brazil dhidi ya Poland usiku wa leo.
Matukio Duniani kupitia mtandao wake rafiki wa Sportsmail
inafahamu kuwa Carrick – ambaye kwa wiki nzima iliyopita alipewa jukumu
la kufanya mazoezi kwenye kiungo ndani ya dimba la mazoezi la mtakatifu
St George’s Park na anatarajia kucheza safu ya kiungo na nahodha wa
Liverpool na timu ya Taifa ya England, Steven Gerrard .
Kiwango
cha Carrick kilianza kulivutia benchi la ufundi la England baada ya
kuonesha soka safi katika mchezo wa mwisho wa klabu yake ya Manchester
United dhidi ya Sunderland ambapo waliibuka na ushindi.
Hakuna
maajabu, anafurahi tu: Michael Carrick amepewa nafasi muhimu ya
kuitumikia England usiku wa leo katika mchezo muhimu zaidi wa kuwania
kufuzu fainali za kombe la Dunia mwakni nchini Brazil dhidi ya Poland
uwanja wa Wembley
Nje: Frank Lampard alianza dhidi ya Montenegro, lakini hataanza leo dhidi ya Poland
Kocha
Hodgson anatarajiwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao ulimpa ushindi wa
mabao 4-1 dhidi ya Montenegro ijumaa iliyopita katika dimba la Wembley,
na nyota wake Andros Townsend yuko sawa kuanza mechi ya leo.
Carrick
aliingia akitokea benchi na kuchukua nafasi ya Lampard dakika ya 65
siku ya Ijumaa iliyopita na wakati huo England ilikuwa mbele kwa mabao
2-0.
Nafasi
nyingine: Kocha wa England, Roy Hodgson (chini) anatarajiwa kwa mara
nyingine kumuanzisha Andros Townsend baada ya kuonesha kiwango kikubwa
dhidi ya Montenegro
Ushindi lazima: Endapo England watashinda leo wanaweza kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani nchini Brazil
0 comments:
Post a Comment