JOSEPH
Owino amewaambia mastraika wa Simba kwamba yeye atakuwa makini sana
kwenye ulinzi kuikabili Yanga na wao wapige mabao ya haraka haraka.
Lakini wachezaji watano kati ya 11 wa Simba watakaoishukia Yanga Jumapili ijayo ni wapya kabisa.
Wachezaji hao walioko kwenye
kambi ya Simba, Kigamboni, Dar es Salaam ni kipa Abel Dhaira na beki
Joseph Owino ambao ni raia wa Uganda, Warundi Gilbert Kaze na Amisi
Tambwe na mshambuliaji wa Tanzania, Betram Mwombeki.
Dhaira, Owino, Tambwe, Kaze na
Mwombeki ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba na ambao
wamejihakikishia namba kwenye timu hiyo inayofundishwa na Kocha Abdalah
Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo.
Mbali na wachezaji hao
wanaofanya vizuri, kikosi cha Simba kitawakosa wachezaji sita waliocheza
pambano la mzunguko pili msimu uliopita dhidi ya Yanga lililopigwa Mei
18 na Yanga kushinda 2-0.
Wachezaji hao ni kipa Juma
Kaseja, mshambuliaji Felix Sunzu, mabeki Shomari Kapombe, Mussa Mude na
viungo Mrisho Ngasa na Mwinyi Kazimoto.
Wakati Kaseja na Sunzu mikataba
yao ilimalizika, Mude alikatishwa mkataba, Kapombe alitimkia Ufaransa
kufanya majaribio ya soka la kulipwa kama ilivyo kwa Kazimoto
aliyekwenda nchini Qatar, huku Mrisho Ngasa akihamia Yanga.
Hata hivyo,Yanga inayonolewa na
kocha wake yule yule Mdachi Ernest Brandts inatarajia kushuka uwanjani
na wachezaji 10 kati ya 11 waliocheza mechi dhidi ya Simba Mei 18 huku
Simba pia ikiwa imemtimua kocha wake wa kipindi hicho, Patrick Liewig
raia wa Ufaransa.
Mchezaji pekee kwenye kikosi cha
Yanga ambaye atacheza mchezo huo kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa
ni Ngassa mwenye mabao mawili miongoni mwa vinara wa kutikisa nyavu
katika Ligi Kuu msimu huu.
Katika hatua nyingine, Owino
amesema kuwa: “Kwa upande wetu tuko vizuri, mimi na mwenzangu, Kaze
hakuna shida tumekamilika, lakini mechi yetu na Yanga kulingana na
uzoefu wangu wa miaka mingi ina changamoto nyingi.”
“Nimewaona Yanga wanavyocheza
ukilinganisha na sisi tunavyocheza nashindwa hata kutabiri naona
atakayelala vizuri na kuamka na bahati atashinda, tunatakiwa kucheza
vizuri, kuhakikisha tunafunga mabao mapema ili kucheza kwa
nafasi,”alisema.
Mechi
ya Simba na Yanga huwa na ushindani mkubwa kutokana na upinzani wa
miaka mingi wa timu hizo na katika maandalizi yao, Simba wamejificha
ufukwe wa Bamba na Yanga wapo Pemba.
CHANZO: MWANASPOTI
0 comments:
Post a Comment