Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Mchezaji ghali zaidi katika Ulimwengu wa soka, Gareth Bale atakaa nje ya dimba kwa wiki tatu kabla ya kuwa fiti kucheza mechi ya kwanza kwake baina ya watani wa jadi wa La Liga, klabu yake ya ReaL Madrid dhidi ya Fc Bracelona maarufu kwa jina la Clasico.
Nyota huyo raia wa Whales tangu ajiunge na miamba hiyo alianza mechi moja tu kati ta tano alizoichezea Real Madrid na amekaa uwanjani dakika zipatazo 132 katika michezo yote. Na bado anasubiri kuanza kwa mara ya kwanza katika mechi ya nyumbani.
Leo hii usiku katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baina ya Copenhagen, Bale alitaraji kucheza mchezo wake wa kwanza nyumbani, lakin itakosa kipute hicho kutokana na majeruhi na atakaa nje kwa wiki tatu kabla ya kucheza mchezo dhidi ya Barcelona Octoba 27 mwaka huu.
Anaumwa: Gareth Bale akiwasili leo hospitali ya Madrid kuchukua vipimo
Bado sana: Bale alitakiwa kuanza katika mechi dhidi ya Getafe, lakini alishindikana wakati wa mazoezi ya kupasha moto misuli
Ngoma inaendeshwa: Bale (kushoto) akiwa amekaa kiti cha abiria wakati akiwasili kuchukua vipimo
Chini: Bale alianzia benchi katika mchezo wa watani wa jadi , klabu ya Atletico Madrid
Mwanzo mzuri: Bale alifunga kwa mara ya kwanza na kuisaidia Real Madrid katika ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Galatasaray.
0 comments:
Post a Comment