Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
WAKATI
homa ya pambano la watani wa jadi, Simba Sc na Yanga ikizidi kushika
kasi na habari ya mjini ikiwa ni hadithi juu ya mechi hiyo ya kukata na
shoka, wadau wazidi kutathmini kipute hicho kitakachopigwa kesho (Octoba
20 mwaka huu) uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Asubuhi hii, mtandao wa MATUKIO DUNIANI umekutana
uso kwa uso na beki wa zamani wa Yanga na sasa mchambuzi na soka
nchini, Ally Mayay Tembele, ambaye kwa upande wake amesema mechi ya
kesho ni ngumu kwa timu zote licha ya watu wengi kuamini kuwa
wanajangwani wana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea kwa madai ya kuwa na
kikos imara na kilichodumu kwa muda mrefu.
“Mechi
za Simba na Yanga si rahisi kutabiri, unaweza kusema labda Yanga ni
bora zaidi ya Simba au Simba ni zaidi ya Yanga, lakini aliyebora zaidi
ya mwenzake kwa wakati huo akashindwa kupata matokeo ya uwanjani,
kwahiyo ni kusubiri kuona nini kitatokea uwanjani”. Alisema Mayay ambaye
alikuwa beki wa zamani wa Yanga.
Mayay
aliongeza kuwa kuna wakati Yanga SC waliwahi kufukuza wachezaji
takribani wote na wakatumia kikosi B, na Simba SC wakawa na imani kubwa
ya kuwafunga, lakini hadi dakika tisini zinamalizika, matokeo yalikuwa
sare.
Beki
huyo aliyekuwa na sifa ya kucheza soka safi na kukaba kwa akili enzi
zake, aliongeza kuwa kwasasa Yanga wanaonekana kuwa na kikosi kizuri
zaidi ya Simba SC na watani wao wana kikosi kizuri pia na kipya achilia
mbali wachezaji wachache waliokuwepo mechi iliyopita mei 18 mwaka hii
akiwemo Amri Ramadhan Kiemba na Masud Nassor Cholo, lakini katu hawezi
kutabiri nani atakuwa mshindi kwani soka la klabu hizo ni gumu kutabiri.
Ally
Mayay Tembele waliochuchumaa chini (wapili kulia) enzi zake akiitumika
klabu ya Yanga, alikuwa beki makini mno na sasa ni moja kati ya
wachambuzi wazuri wa soka la Tanzania.
“Mimi
hata ukinikuta njiani, ghafla ukaniuliza, nani ataibuka na ushindi
kesho?, sitaweza kukupa utabiri hata kidogo zaidi ya kukwambia tusubiri
dakika 90, kwani hizi timu mbili wewe zisikie tu”. Alisema Mayay.
Akizungumzia
uzoefu wake alioupata wakati akichezea timu ya Yanga, Mayay alisema
wachezaji wanapoingia uwanjani kwenye mechi ya watani wa jadi,
wanatafuta zaidi ya matokeo ya ushindi, kwani wanaingia kwa kukamia ili
kuonesha ubora wao kwa mashabiki.
“Zinapokana
timu hizi, wachezaji wanajituma zaidi na kuonesha kiwango chao,
wanatafuta ushindi kwa nguvu zote kwani ndio sifa yao ukizingatia hizi
ndizo klabu kubwa zaidi hapa nchini, binafsi nitaingia uwanjani kwa
kusuburi dakika za mwamuzi”. Alisema Mayay.
Katika
mchezo wa kesho, Yanga itaingia na wachezaji wengi waliocheza mechi ya
mei 18 mwaka huu ya kufunga dimba la ligi kuu soka Tanzania bara ambapo
Simba walilala kwa mabao 2-0.
Yawezekana
wachezaji kama Ally Mustapha `Bartez`, Mbuyu Twite, Nadir Haroub
`Canavaro`, Kelvin Yondan, Athumani Idd `Chuji`, Haruna Niyonzima,
Didier Kavumbagu, Jerry Tegete, Hamis Kiiza, Saimon Msuva wataanza, pia
kutakuwa na ongezeke la David Luhende ambaye kwa wakati ule hakuaminiwa
kama sasa, atakuwepo Mrisho Ngassa ambaye alikuwa Simba na wengine
wengi.
Kikosi
cha Simba asilimia kubwa ni wapya na hawakuwepo, mfano ambao
hawakucheza na hawakuwepo ni Abel Dhaira, Issa Rashid, Gilbert Kaze,
Joseph Owino Gella, Betram Mwombeki, Hamis Tambwe, Henry Joseph, ila
pia watakuwepo vijana waliotoka kikosi B, Harun Chanongo, Jonas Mkude,
Ramadha Singano, William Lucian `Gallas` na wengineo.
Baadhi
ya wachezaji muhimu wa Simba sc msimu ulipita hawapo, mfano Nahodha
wake Juma Kaseja aliyemaliza mkataba na kalbu, Juma Nyoso, Haruna Moshi
`Boban` wote wapo coastal Union, Amir Maftah, Emmanuel Okwi, Ferlix
Sunzu, Musa Mude, Shomary Kapombe na wengineo.
Kwahiyo
unaweza kusema Simba sc mpya inaenda kukabiliana na Yanga ileile ya
Zamani, dakika 90 zinasubiriwa kwa hamu kubwa kuona nani ataibuka na
pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa kesho..
0 comments:
Post a Comment