Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya
Wanafunzi wa Sekondari za Chanzige na Kimani Wilayani Kisarawe Naibu
Waziri Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa mkutano kati ya
Wananfunzi, Watendaji wa Halmashauri na Madiwani, Katikati ni Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe Mhe. Fatma Kimario Mhe.Ummy Mwalimu akiwasalimia watoto wanaosoma katika Shule ya Awali ya Mtakatifu Stephano Shahidi, alipowatembelea jana
Mhe.
Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na watoto wa shule ya awali ya
Mtakatifu Stephano Shahidi,Wakuu wa Shule hiyo,Walimu na Baadhi ya
Watendaji wa Halmashauri
…………………
Na Asteria Muhozya, Pwani
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ameanza
Ziara yake MKoa wa Pwani katika Wilaya za Kisarawe,Rufiji, Mkuranga, na
Mafia ambapo anatarajia kutembelea Utekelezaji wa Miradi na Shughuli za
Maendeleo ya Jamii Mkoani humo.
Katika Ziara yake jana Mhe.Ummy amepata nafasi ya kukutana na Watendaji
Wakuu wa Wilaya ya Kisarawe ambapo taarifa ya utekelezaji wa Wilaya imewasilishwa kwake, Vilevile amefanya kikao na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii , Amekutana na Wananfunzi wa Sekondari za Kimani na Chanzige, na ametembelea Shule ya Watoto ya Awali ya Mtakatifu Stephano.
0 comments:
Post a Comment