Docta
Yasin Hamza akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja kati ya wanafunzi wa
Skuli za Maandalizi katika maadhimisho ya Afya ya mtoto yaliyofanyika
Kijiji cha Chwaka.Wanafunzi wa Skuli za Maandalizi Chwaka na Jendele wakionyesha michezo katika maadhimisho ya siku ya Afya ya Mtoto
Mgeni
Rasmin wa maadhimi ya siku ya Afya ya mtoto Mussa Mwadini Mcha
akizungumza na Wazazi na Walezi wa skuli za Maandalizi. kuliani kwake
Mratibu wa Jumuiya ya Skuli za Maandalizi za Madrasa Mohamed Othman na
kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Skuli ya Maandalizi ya Madrasati Maamur
ya Chwaka.
Picha na Ramadhan Ali wa Maelezo Zanzibar.
Na Ali Issa na Miza Othman Maelezo-Zanzibar
Wazazi
na Walezi wa vijiji vya Chwaka na vijiji vya jirani wameshauriwa
kuwapeleka watoto wao Skuli za Maandalizi mapema wakiwa na umri wa
miaka mitatu ili kuwajengea uwezo wa ufahamu wakiwa bado wadogo.
Hayo
yameelezwa leo na Katibu wa Kamati ya Maendeo ya kijiji hicho Mussa
Mwadini Mcha wakati alipokuwa akizungumza na wazazi na wanafunzi wa
skuli za maandalizi za vijiji vya Chwaka na Jendele katika Madhimisho
ya siku ya Afya ya Mtoto zilizoandaliwa na Zanzibar
Madrasa Resouce Centre (ZMRC) zilizofanyika kijijini hapo.
Amesema
kumpeleka mototo skuli katika umri huo ni kumkuza kiakili na kimwili
na hatimae katika umri wa utuuzima mtoto huyo huwa na ufahamu mkubwa.
“Nivizuri
kumpeleka skuli mtoto akiwa na umri wa chini ya mika minne kwani
kufanya hivyo inampelekea mototo kuwa na akili nzuri na kumuandaa
mapema na elimu ya msingi,” alisema Mussa Mwadini.
Aidha
aliwafahamisha wazee hao kuwapatia watoto chakula mchanganyiko chenye
kujenga mwili ili wawe na Afya na ukuaji na kukua vizuri.
Nao
walimu wa Madrsa hizo walielezea changamoto zinazo wakabilikatika skuli
zao ikiwemo uhaba wa vikalio, vifaa vya kusomea na kukosa uzio katika
skuli zao ambapo baadhi ya watu huingia na waharibifu na kuharibu
mazingira ya skuli zao.
“Uzio
ni tatizo kubwa katika skuli zetu za maandalizi na mara nyingi
tunashindwa kuweka pembea za kuchezea kwa kuhofia kuharibiwa na watu
wasiopenda maendeleo yetu”,alisema Batuli Abdi Mwalimu wa Skuli ya
Jendele.
Hata
hivyo walimu hao wamelalamikia ushirikiano mdogo kati yao na wazazi
wa wanafunzi wakati wanapoitwa katika Madrasa hizo jambo ambalo
linarudisha myuma maendelea kwa walimu na wanafunzi wao.
0 comments:
Post a Comment