Wednesday, September 11, 2013


Na Baraka Mpenja, Mbeya
HOMA ya pambano la jumamosi baina ya Mbeya City dhidi ya mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga katika uwanja wa sokoine jijini hapa  inazidi kupanda moto huku kila kona hadithi kubwa ikiwa ni mechi hiyo.
Wakati mechi hiyo inazidi kutawala midomoni mwa watu, vijana wa Mbeya City wanazidi kujiimarisha zaidi kuelekea mchezo huo ambapo wanaendelea na mazoezi yao katika uwanja wa sokoine chini ya kocha Juma Mwambusi.
Mwambusi mwenye uzoefu na ligi kuu itaiongoza timu yake hiyo ambayo ni mara ya kwanza kukabiliana na Yanga, huku akiwa na matumaini ya kuwaadabisha wana jangwani hao wanaotamba kuwa timu bora na mabingwa watarajiwa wa ligi kuu msimu wa 2013/2014.
“Tunawaheshimu sana Yanga, ni klabu kubwa na yenye uzoefu mkubwa, lakini sisi tumejiandaa kucheza na timu zote 13, hivyo hatujali kama ni Yanga au nani, kikubwa tuko vizuri na tunahitaji ushindi ili kuendelea kujiweka sehemu nzuri”. Alisema Mwambusi baada ya mazoezi ya timu yake.
e76dYanga1 
Wakati huo huo kikosi cha wanajangwani chini ya kocha wake, Mholanzi, Ernie Brandts kinatarajiwa kuwasili leo jijini Mbeya tayari kwa mawindo yake ya mechi hiyo yenye mvuto wa aina yake kwa mashabiki wa kandanda.
Wachezaji ambao wapo safarini ni Makipa: Ally Mustafa ‘Barthez’, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Yusuph Abdul,.
Walinzi:  Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub `Cannavaro`, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kevin Yondan,  Rajab Zahir , Issa Ngao na  Ibrahim Job.
Viungo ni Athuman Idd ‘Chuji’, Salum Telela, Frank Domayo, Haruna Niyonzima `Fabregas`, Nizar Khalfani, Hamisi Thabit na Bakari Masoud.
 Wakati washambuliaji ni Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Abdallah Mguhi, Didier Kavumbagu, Jerry Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Shaban Kondo na Reliants Lusajo.
DSC_03521 
Mbeya City tayari wameshashuka dimbani mara mbili katika uwanja wao wa nyumbani ambao mechi ya kwanza ilichezwa agosti 24 dhidi ya Kagera Sugar na walitoka suluhu, huku mechi ya pili wakishinda mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Nao Yanga wamekipiga mara mbili huku mechi ya kwanza wakishinda kwa mabao 5-1 dhidi ya Ashanti United, na mechi ya pili wakatoka sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video