Wednesday, September 4, 2013


Na Baraka Mpenja , Mbeya
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Klabu ya Yanga, wamewafagilia  wanandinga   wao  kwa kutekeleza majukumu yao na ndio maana wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanatetea taji lao walilotwaa msimu uliopita, huku wakimaliza ligi kuu kwa kuwateketeza watani wao wa jadi, Simba SC kwa mabao 2-0.
Afisa habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto amezungumza na mtandao wa MATUKIO DUNIANI na kuweka wazi kuwa kwa sasa wanaendelea na mazoezi ya kujipanga kuelekea mchezo wa septemba 14 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
“Yanga ndio mabingwa watetezi, washindi wa kikombe cha ngao ya jamii, mabingwa watarajiwa wa ligi kuu msimu huu, hivyo kazi ni moja tu, tunapambana na kujipanga kufanya vizuri zaidi, na kikubwa kinachotia moyo ni uwezo mkubwa wa kikosi na morali ya hali ya juu”. Alisema Kizuguto.
IMG_7295Mechi iliyopita, Yanga walikabwa na Wagosi wa Kaya na pichani juu, Ally Mustafa ‘ Batez’ golikipa wa Yanga akijaribu kumhadaa nahodha wa Coastal Union, Jerry Santo kabla hajapiga penati katika matokeo ya sare ya  1-1
Kizuguto ameongeza kuwa wanatambua Mbeya City imekuja kwa nguvu sana, lakini kwa Yanga bado sana na lazima cheche zao zitazimwa tu wakiwa nyumbani kwao.
Pia amewataka mashabiki wa Yanga,  nyanda za juu kusini kujitokeze kwa wingi kuwaona mabingwa  watetezi  kwani burudani kubwa itaonekana.
“Yanga ni timu ya wananchi, na kila inapocheza mashabiki wanajitokeza kwa wingi, hivyo tunaendelea kuwaomba wazidi kujipanga kuelekea kipute hicho”. Alijigamba Kizuguto.
DSC_0352Kikosi cha Mbeya City kilichotoka suluhu (0-0) na wakali wa Kagera Sugar kutoka Kaitaba katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Agosti 24 Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
Wakati Yanga wakitamba, nao wenyeji wa mchezo huo, klabu ya Mbeya City wamejibu mapigo na kusema wao wamejipaga kupambana na timu zote 13 na si vinginevyo.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Juma Mwambusi amesema wanaendelea kujifua ili kuwakabili wapinzani wao ambao ni timu kubwa zaidi katika soka la Tanzania.
“Yanga wana historia kubwa, tunawaheshimu kwa uzoefu wao, lakini sisi tumepanda ligi kuu na kujiandaa kucheza na timu zote, hivyo tunajipanga kupata ushindi ili kujiweka mazingira mazuri zaidi”. Alisisitiza Mwambusi.
Mbeya City mpaka sasa wana pointin 4 kwani mechi ya kwanza walitoka suluhu na Kagera Sugar na wakashinda mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting , mechi zote zilichezwa katika dimba la sokoine.
Kwa upande wa Yanga nao wana pointi 4 ambapo walishinda mabao 5-1 dhidi ya Ashanti United na kutoka sare ya 1-1 na Coastal union, mechi zote zilichezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kwa mara ya mwisho Yanga kucheza Mbeya ilikuwa septemba 15 mwaka jana ambapo walicheza mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons na kutoka suluhu. Na baada ya mechi kocha wao kwa wakati ule, Tom Saintfiet alikaririwa akilalamikia ubovu wa uwanja na hoteli mbaya za mbeya kuwa chanzo cha kupoteza mechi hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video