Na Baraka Mpenja , Mbeya
MIKIKIMIKIKI
ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 inatarajiwa kuendelea
kushika kasi wikiendi hii (Jumamosi na jumapili), huku macho ya
mashabiki wengi wa soka wakisubiri kuona nini mabingwa watetezi, Klabu
ya Yanga watafanya dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa baada ya
kukubali kichapo cha mabao 3-2 wiki iliyopita kutoka kwa Azam Fc.
Yanga
wanatarajiwa kushuka dimbani hapo kesho (septemba 28) katika dimba lao
la nyumbani dhidi ya vijana wa Charles Boiface Mkwasa `Master`, huku
wakiwa na pointi 6 tu katika nafasi ya 8 ya msimamo.
Wanajangwani
wataingia uwanjani wakiwa na machungu ya kufanya vibaya mechi za nyuma
na tayari mwenyekiti wa klabu hiyo, Yufus Manji amewataka wachezaji
kutulia na kuwasisitiza kuwa hana tatizo nao kutoakana na matokeo
mabaya.
Sakata
la Ngassa lilianzia Agosti mwaka jana alipoupandisha hasira uongozi wa
iliyokuwa klabu yake, Azam FC kwa kwenda kubusu jezi ya Yanga SC baada
ya kufunga bao la ushindi katika Nusu Fainali ya Kombe la Kagame dhidi
ya AS Vita ya DRC, Uwanja wa Taifa.
Mwenyekiti wa Simba Sc, Aden Rage hataki fedha za mafungu mafungu kutoka kwa Ngassa
Wakati
huo huo, Uongozi wa Simba Sc kupitia kwa mwenyekiti wake, Alhaj Ismail
Aden Rage umetoa msimamo wake kuwa Ngassa anatakiwa kulipa fedha zote na
hawako tayari kupokea kwa mafungu mafungu kama walivyofanya wakati wa
sakata la Mbuyu Twite.
Rage
ametoa tahadhari hiyo huku akisema wao wanapenda nyota huyo acheze
soka, lakini wanataka mzigo wote na si nusu nusu, vinginevyo
hawatakubali.
Lakini
amesisitiza kuwa Ngassa hajaomba kulipa kwa mafungu, ila wamelazimika
kutoa msimamo huo kwani fedha ya mafungu mafungu huwa zinatibua bajeti
yao kama ilivyotokea kwa mzigo waliolipwa na Yanga wakati wa sakata la
beki Mbuyu Twite aliyekula fedha za Simba na kisha kusaini Yanga.
Kikosi cha Mbeya City
Mbali
na mechi hiyo, kipute kingine cha kuvutia kitakuwepo katika dimba la
Sokoine hapa jijini Mbeya ambapo wakali wanaotikisa na kugonga akili za
wapenzi wengi wa soka nchini, klabu ya Mbeya City itakuwa kibaruani
kumenyana na Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga.
City
waliopo nafasi ya 7 wakijikusanyia pointi 7 watashuka dimbani mbele ya
Wagosi wa Kaya wenye pointi 9 katika nafasi ya 5 ili kusaka ushindi wa
pili uwanja wa nyumbani.
Ikumbukwe
kuwa hiyo itakuwa mechi ya nne kwa Mbeya City kucheza nyumbani, ambapo
alianza mechi ya ufunguzi na Kagera Sugar, ikacheza na Ruvu Shooting na
hatimaye na Yanga kabla ya kwenda Manungu kucheza na Mtibwa Sugar na
kuingia Dar es salaam kukipiga na Simba.
Kati ya mechi hizo za nyumbani ilishinda moja tu dhidi ya Ruvu shooting kwa mabao 2-1 na nyingine iliambulia suluhu na sare.
Huko
uwanja wa A.H. Mwinyi, Maafande wa jeshi la wananchi (JWTZ), Rhino
Rangers watakuwa wenyeji wa `Wanankulukumbi`, Kagera Sugar.
Mechi
nyingine itawakutanisha Mgambo JKT katika dimba la Mkwakwani dhidi ya
Maafande wa jeshi la kujenga Taifa, JKT Oljoro kutoka mjini Arusha.
Mitanange ya Ligi hiyo itaendelea jumapili kwa mechi tatu kupigwa katika viwanja Tofauti.
Vinara
wa ligi hiyo wenye pointi 11, wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa
ugenini katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam kukabiliana na
maafande wa JKT Ruvu FC waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 9
kibindoni.
Nao vibonde Ashanti United watakuwa kibaruani kupepetana na Mtibwa Sugar uwanja wa Azam Complex.
Maafande
wa Tanzania Prisons `Wajelajela` watakuwa mzigoni kusaka pointi tatu
muhimu mbele ya wana Lambalamba, Azam C katika uwanja wa Soine jijini
Mbeya.
0 comments:
Post a Comment