CHAMA CHA WAZAZI WA WATOTO WENYE ULEMAVU WA MTINDIO WA UBONGO, AKILI NA VIUNGO TANZANIA. (CHAWAUMAVITA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SIKU YA CP DUNIANI JUMATANO OKTOBA 2 2013-
WORLD CELEBRAL PALSY DAY
Chama cha
Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo
Tanzania (CHAWAUMAVITA) ni chama kilichoanzishwa mwezi MACHI mwaka 2013.
namba ya usajili ni S.A 18732.
Dira
ya CHAWAUMAVITA ni kuwa CHAMA cha mfano kitachochangia upatikanaji wa
huduma bora na endelevu kwa watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,
akili na Viungo Tanzania ili kuhakikisha watoto wenye Ulemavu wa Mtindio
wa Ubongo, akili na Viungo wanasaidiwa kimaono, kimwili, kiroho,
kiakili, kijamii, kimawazo na kuandaa mazingira bora ya makuzi na maisha
yao kwa ujumla
Chawaumavita
inautaarifu umma kuwa Jumatano ya Oktoba 2, 2013 ni siku ya CP duniani
ambapo mataifa mbalimbali(www.worldcpday.com) yakiongozwa na umoja wa CP
–united Celebral palsy –wataadhimisha siku hiyo kimataifa, ambapo kauli
mbiu ya mwaka huu ni
“CHANGE MY WORLD IN 1 MINUTE”
Inasadikiwa
kuwa kuna jumla ya watu milioni kumi na saba (17.000.000) duniani wenye
CP. Msanii mashuhuri mlemavu aliyejizolea sifa katika filamu-series- ya
BREAKING BAD JM Milly ameteuliwa kuwa balozi wa watu wenye CP
duniani,msanii huyo ambaye ni miongoni mwa watu wenye CP ameonyesha
kuwa CP sio kikwazo katika kumfanya mtoto aliyepata CP kushindwa kufikia
malengo yake.
Ripoti inaonyesha katika kila watoto 3 wenye CP 1 hawezi kutembea,na kila watoto 4 wenye CP moja hawezi kuongea
Hivyo
basi CHAWAUMAVITA inatoa wito kwa wazazi,familia,jamii na Taifa kwa
pamoja kuhakikisha tunajenga mazingira ya kuwawezesha watoto/watu wenye
CP Tanzania wanafikia malengo.
CHAWAUMAVITA katika kuadhimisha siku hii duniani imeamua kufanya yafuatayo:
- UFUNGUZI rasmi wa ofisi iliyopo sinza katika kiwanja cha kinesi
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwako..
Pamoja na salaam zetu za Pamoja Tunaweza,
Wako,
Bw Jonathan KAWAMALA.
MWENYEKITI
SEPTEMBA 16, 2013.
0 comments:
Post a Comment