Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MSHAMBULIAJI wa Asernal, Olivier Giroud amepunguza hofu juu ya majeruhi aliyoyapata juzi katika mchezo dhidi ya Sunderland.
Nyota huyo alitolewa nje dakika za mwisho na kocha Arsene Wenger alikiri kuwa na wasiwasi ya kumkosa mshambuliaji wake pekee ambaye yuko fiti katika kikosi chake.
Lakini
mkali huyo raia wa Ufaransa ambaye amefunga kila mchezo wa ligi kuu
msimu huu amesema kuwa anaweza kuwa fiti katika mchezo muhimu wa
ufunguzi wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya
Marseille jumatano.

Niko
fiti: Kulikuwa na wasiwasi kuwa majeruhi aliyoyapa Olivier Giroud
katika mchezo dhidi ya Sunderland yangemweka nje ya uwanja jumatano ya
wiki hii

Hali mbaya: Arsene Wenger alikuwa na shaka kuwa atamkosa mshambuliaji wake pekee katika mchezo wa keshokutwa jumatano
Santi
Cazorla anatakiwa kuwa nje hadi katikati ya Oktoba na alipoulizwa juu
ya maumivu yake, Giroud alisema: “Si mbaya hakika, si mbaya kama
nilivyohofia awali. Nilipata pigo mapema mchezoni, lakini hakuna
aliyekuwa karibu yangu wakati naumia wakati huo,”alisema.
“Nilikuwa
nawania mpira nikadondokea mguu. Nikaumia kifundo cha mguu, lakini
bahati nzuri, hakuna maumivu makubwa. Nipo vizuri, kweli nitakuwa safi
(kwa mechi na Marseille),”.
Giroud
anatakiwa kutambua ukweli kwamba alisajiliwa baada ya kuondoka kwa
Robin van Persie Emirates msimu uliopita, na kiwango chake kinaenda
kikikua tangu msimu uliopita.
Ameanza
vizuri msimu huu na kuna matumaini atafanya vizuri zaidi hasa baada ya
kusajiliwa kwa kiungo Mjerumani, Mesut Ozil kwa dau la Pauni Milioni
42.5 kutoka Real Madrid.


Yuko kwenye kiwango: Giroud amefunga katika kila mchezo wa ligi kuu msimu huu

Msaidizi wa nguvu: Lakini amesema kazi yake imekuwa nyepesi kwa kucheza na mchezaji kama Mesut Ozil (kulia)
0 comments:
Post a Comment