Profesa Mark Mwandosya |
WAZIRI
wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya
amesemwa Tanzania itafikia maendeleo ya hali ya juu ifikapo mwaka 2025
hadi mwaka 2030 ikiwa watu watafanyakazi kwa upendo, uzalendo na
kujiamini.
Aidha
Profesa Mwandosya amesema kwamba Serikali inajitahidi kufikisha huduma
zake kwa karibu na wananchi, licha ya kuwepo kwa changamoto za kielimu
na miundombinu, lakini mambo mengi yanafanyika,hivyo wenye macho
wanaona.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Profesa Mwandosya wakati hafla fupi ya
kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya
chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya Sh.
milioni 38 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam.
“
Mimi nina matumaini makubwa na nchi yetu ifikapo mwaka 2025 hadi 2030
tutakuwa ni nchi yenye watu wenye kipato cha kati.Pia ifikapo mwaka 2050
nchi yetu itakuwa imeendelea hakutakuwa na mtu mwenye kipato cha kati
wala cha chini kama ilivyo nchi ya Singapore,” alisema Profesa
Mwandosya.
Profesa
Mwandosya aliongeza kuwa gari hilo ni moja ya juhudi za Serikali za
kuhakikisha kuwa huduma zake zinaifikia jamii kila mahali hususan
kwenye maeneo ya vijijini.
“Serikali
inajitahidi kufikisha huduma zake mfano katika sekta ya elimu kuna
mambo mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika ikiwemo katika sekta
nyingi kama vile kwenye nishati gesi tunakwenda vizuri. Tukisimamia
vizuri rasilimali zetu ,basi hata huduma tutazifikisha vizuri kwa
wananchi,” alisisitiza.
“
Kila mtu duniani anasema Tanzania inapiga kasi katika kuwaletea
maendeleo wananchi . Mimi nadhani hatutarudi nyuma. Wale wanaopiga
kelele hautajafanya kitu ,lakini mwenye macho wanaona,” alisisitiza
Profesa Mwandosya.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Charles Pallangyo akizungumzia
kuhusu gari hilo alisema litasaidia kuhimarisha huduma za chanjo katika
halimashauri hiyo na kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito na
watotowenye umri wa chini ya miaka mitano ili kutimiza malengo ya
millinea ya namba 4na 5 ifikapo mwaka 2015.
Naye
Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando alisema nchi hivi sasa
imefikia wastani wa asilimia 92 katika huduma za chanjo kutoka asilimia
90 ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mwenyekiti
wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga aliishukuru wizara hiyo kwa
msaada huo ,ambapo alisema gari hilo litatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa ili kuinua kiwango cha huduma hiyo kwenye eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment