Tuesday, September 3, 2013

IMG_1289WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania itasimamia vizuri miradi iliyoanzishwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekani na kuhakikisha inakalimika ili iweze kuwanufaisha wananchi waishio kwenye maeneo ya hiyo miradi.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Septemba 3, 2013) wakati alipokutana na Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake hapa nchini, Bw. Alfonso Lenhardt ofisini kwake Bungeni, Dodoma.
 
Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa kuiwezesha Tanzania kunufaika na miradi mingi ya kimaendeleo katika kipindi ubalozi huo ulipokuwa chini ya uongozi wake.
 
“Miradi uliyoiasisi ni mingi, na kazi uliyoifanya ni kubwa mno. Nimeorodheshewa idadi ya miradi iliyofanyika wakati ukiwa madarakani, kwa kweli ni mingi na orodha ni ndefu mno, tunakushukuru sana,” alisema.
 
Alisema Serikali inapitia upya miradi ya barabara iliyo chini ya MCC ili iweze kunufaisha wakazi wa vijijini kwa kufungua maeneo yao kiuchumi na kuwawezesha kupata masoko kwa urahisi.
 
Alisema mbali ya barabara, Serikali pia imepania kuboresha upatikanaji wa umeme vijijini na wilayani ili kuwezesha uanzishaji wa viwanda vidogo vua usindikaji. “Lakini jambo hili haliwezi kufanikiwa kama sekta binafsi haitakuwa na mchango mkubwa katika suala hili,” alisema Waziri Mkuu.
 
Marekani imeisadia Tanzania kwenye miradi ya kuongeza lishe kwenye chakula, kupambana na malaria, afya ya mama na mtoto, UKIMWI, kilimo, barabara na nishati.
 
Kwa upande wake, Balozi Lenhardt alimweleza Waziri Mkuu kwamba amefurahia kipindi chote cha miaka minne ambacho yeye na mke wake waliishi hapa nchini na kwamba anaamini Serikali ya Tanzania itahakikisha miradi yote inayofadhiliwa na nchi hiyo, inakamilika.
 
Alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba miradi yote iliyoanzishwa chini ya uongozi wake itakamilika na kwamba ana hakika kwamba upatikanaji wake wa fedha hautatetereka kwa sababu yeye anaondoka nchini.
 
Alisisitiza haja ya sekta binafsi nchini kuhakikisha inashirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
 
Alimkabidhi Waziri Mkuu zawadi ya sarafu maalum (coin of excellence) ambayo hutolewa kwa watu ambao utendaji kazi wao umetia fora na kumweleza kwamba anatambua mchango wa Waziri Mkuu kwa Taifa hili katika kusukuma suala la kilimo.
 
Sarafu hiyo ina bendera za Marekani na Tanzania, ina ramani ya Ziwa Victoria na mazao
 
Waziri Mkuu alimshukuru sana kwa zawadi hiyo na hasa kwa maana kubwa ambayo sarafu hiyo imebeba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video