Askari
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Leonard Mponeza akiwaelekeza watendaji
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jinsi ya kutumia mitungi ya kuzimia
moto. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi.
Mafunzo hayo ya Kinga na Tahadhari ya Moto yalitolewa katika Ukumbi wa
Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili
kulia) pamoja na watendaji wa wizara hiyo wakiingalia kwa makini chupa
yenye dawa ya kuweka kwenye mitungi ya kuzimia moto. Kulia ni askari wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Leonard Mponeza ambaye alitoa mafunzo ya
Kinga na Tahadhari ya Moto kwa maofisa hao katika Ukumbi wa Mikutano wa
wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi). Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Lilian Mapfa akizima moto kwa utaalamu baada ya kupata mafunzo ya
Kinga na Tahadhari ya Moto yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
0 comments:
Post a Comment