Aserne
Wenger hajaingia hasara hata kidogo kumnunua Mesut Ozil kutoka Real
Madrid majira ya kiangazi kwani ameendelea kulipa Pauni Milioni 43
zilizotolewa na kumfanya kuwa mchezaji ghali wa klabu ya Arsenal baada
ya kutoa pasi zote za mabao matatu, wakatiThe Gunners ikishinda 3-1
dhidi ya Stoke City na kupanda kileleni uwanja wa Emirates na kubarizi
kileleni mwa ligi kuu soka nchini England.
Aaron
Ramsey alifunga bao lake la saba msimu huu dakika ya tano baada ya
kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Ozil, lakini Geoff Cameron
akaisawazishia Stoke dakika ya 26.
Ozil
akadhihirisha yeye ni mkali, baada ya mpira wa kona aliopiga
kuunganishwa kimiani kwa kichwa na Mjerumani mwenzake, beki Per
Mertesacker dakika ya 36 kuipa Arsenal bao la kuongoza.
Vinara wa ligi: Aaron Ramsey akishangilia bao lake lililowawezesha Arsenal kuwa kileleni
Ni mabao tu : Aaron Ramsey akishangilia bao na wachezaji wenzake baada ya kufunga dhidi ya Stoke leo
Ozil tena akamtengenezea Bacary Sagna nafasi ya kufunga bao la tatu dakika ya 72.
Huu
unakuwa ushindi wa saba mfululizo kwa Arsenal tangu wafungwe 3-1
nyumbani na Aston Villa katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo.
Kikosi
cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs,
Flamini, Wilshere/Monreal dk73, Ramsey, Gnabry/Ryo dk73, Ozil/Arteta
dk81, Giroud.
Stoke: Begovic,
Cameron, Shawcross, Huth, Pieters/Palacios dk67, Wilson, N’Zonzi,
Adam/Ireland dk59, Walters, Arnautovic, Jones/Pennant dk75.
Mwenendo mzuri: Ramsey akishangilia bao lake
Mtanikoma: Charlie Adam akishangilia na mfungaji wa bao la Stoke Geoff Cameron na ubao kusomeka 1-1
0 comments:
Post a Comment