Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam.
SERIKALI inayoendesha mambo yake kwa uwazi inatimiza sharti la msingi la utawala bora kwa kuwajibika ipasavyo kwa wananchi wake.
Hayo
yamesemwa leo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw.
Ludovick Utouh wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa vyombo vya
habari na asasi za kiraia kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya CAG na
kuelewa ripoti za Mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali.
Bw.
Utouh amesema kuwa kutokana na ongezeko la matumizi ya ripoti zake kwa
vyombo vya habari na wadau wengine kumekuwa na upotoshwaji mkubwa wa
taarifa kwa namna zinavyotumiwa na wadau mbalimbali, hivyo warsha hiyo
inatoa fursa ya pekee ili kupunguza upotoshwaji huo kwa kuelimishana,
kurekebishana na kusaidiana ili kuzielewa vizuri ripoti hizo na
kuzilipoti kwa usahihi.
“Warsha
hii inalenga kutoa fursa ya kipekee kwa wadau wetu kushiriki na kutoa
mawazo yao ya namna ya kuboresha mahusiano ambayo yataleta ufumbuzi na
wa madai mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na asasi mbalimbali”.
Alisema Bw. Utouh.
Bw.
Utouh ameongeza kuwa ni vema kufahamu madhara juu ya utoaji taarifa za
upotoshwaji ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza baina ya
pande mbili na pia amesema kuwa ana imani kubwa kuwa kila mwanahabari
anatambua umuhimu wa habari na pia kutambua umuhimu wa uwajibikaji na
utawala bora.
“Msiweke madoido, msipambe taarifa ili kwamba zionekane zina mvuto”. Alisisitiza Bw. Utouh.
Aidha,
Bw. Utouh amevitaka vyombo vya habari kwa kushirikiana na asasi za
kiraia kwa pamoja kuhakikisha kuwa kuna mfumo mzuri wa upatakinaji wa
taarifa na utaoji wa taarifa za serikali kwa usahihi.
Warsha
hiyo imefunguliwa leo Landmark Hotel iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam na inalenga kuwajengea uwezo maafisa habari nchini juu ya kazi za
Mdhibiti wa Hesabu za Serikali na juu ya ubora wa upatikanaji wa habari
zilizosahihi na kuziripoti kwa usahihi.
0 comments:
Post a Comment