Waziri
wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akitoa
maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za
vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi
karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Manedeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba wakati akitoa maelezo juu ya kauli
zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii
ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya
habari hapa nchini.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DAR ES SALAAM.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO-Dar es Salaam.
SERIKALI
imeshtushwa na baadhi ya ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi na
baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini ambao unaweza kuleta kuhatarisha
amani na usalama wa Tanzania.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
Sophia Simba leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa
habari ofisini kwake.
Waziri
Simba amesema kuwa kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya vyama
vya siasa vilivyofanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani
zimeishtua Serikali na zinaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii
hususani wanawake, wazee, walemavu na watoto.
Waziri
Simba amesema kauli zilizotolewa na viongozi hao ni pamoja na “Vijana
msikubali wakati wa kufanya mazoezi umefika” kauli hii inahitaji
tafakari na kuhoji kwa makini inawahamasisha vijana kutii, jambo ambalo
linaweza kuwafanya walete vurugu..
Amesema
kuwa kauli hiyo na nyingine zilizotolewa na viongozi hao wa juu wa
vyama hivyo zinazowachochea wananchi kutotii na ni ishara ya uwepo wa
njama mbaya za kuwashawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria
mikononi, kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu.
Aidha, Waziri Simba alisema jamii inahitaji kutafakari juu ya kauli hizo na mustakabali wa Tanzania.
Amesema
kuwa jamii ya Watanzania inatakiwa kutambua kuwa amani na usalama ndio
mtaji namba moja wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia.
Ustawi wa jamii ya Watanzania unahitaji amani, utulivu na usalama.
0 comments:
Post a Comment