Wanajeshi
watatu wa Kenya wameuawa wakati walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya
watu anaoshikiliwa mateka na magaidi wa al Shabab katika jumba lenye
maduka la Wastgate jijini Nairobi.
Askari wengine 8 wanaripotiwa kuwa mahututi baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo yanayoendelea hadi sasa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Jenerali Julius Karangi.
Duru
za Kenya zinaripoti kuwa hadi sasa watu 69 wamethibitishwa kuwa wameuawa
na magaidi wanaoendelea kupigana na vikosi vya jeshi la Kenya katika
jengo la maduka la Westgate.
Wakati
huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohammed amesema
kuwa Wamarekani wawili au watatu na Mwingereza mmoja wamehusika katika
shambulizi lililofanywa na magaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate
jijini Nairobi. Balozi Amina Mohammed amesema washambuliaji hao walikuwa
wakishirikiana na wenzao katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa ajili ya
kuua watu mwishoni mwa wiki mjini Nairobi. Waziri wa Mambo ya Nje wa
Kenya amesisitiza kuwa shambulizi la sasa mjini Nairobi limefanyika
kitaalamu.
CHANZO: RADIO TEHRAN
0 comments:
Post a Comment