Viongozi
hao wakiwa wakielekea kwenye ukumbi kwa ajili ya kushiriki hafla ya
kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bw. Seth Kamuhanda (katikati). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Bi. Siaba Nkinga na kushoto ni Naibu wake Profesa Elisante Ole
Gabriel.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi wa hafla hiyo Bw. Seth Kamuhanda iliyofanyika jijini Dar es
Salaam. Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth
Kamuhanda akihutubia wakati wa hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Siaba Nkinga
akimkabidhi zawadi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Seth
Kamuhanda.
Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth
Kamuhanda (aliyesimama katikati) akiifurahia zawadi aliyopewa na Katibu
Mkuu mpya wa Wizara hiyo katika hafla iliyoandaliwa na Wizara hiyo.
Kushoto ni Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Bi. Siaba Nkinga na kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel. Hafla
hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth
Kamuhanda (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakiangalia
kwa furaha zawadi aliyokabidhiwa Bw. Kamuhanda kwenye hafla ya kuagwa
kwake.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akikabidhiwa zawadi.
Aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth
Kamuhanda (wa tatu toka kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DAR ES SALAAM
Na Eleuteri Mangi.
WAMILIKI
wa vyombo vya habari nchini wameaswa kuwajengea mazingira mazuri
waandishi wa habari wa vyombo vyao ili waweze kuhabarisha umma wa
Watanzania mambo mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchi kwa
kuzingatia weledi wa taaluma yao.
Rai
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake wa kuitumikia
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Seith Kamuhanda jana
alipokuwa anaagwa na watumishi wa wizara hiyo katika hafla iliyofanyika
kwenye Uwanja wa Michezo wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“
Wamiliki wa vyombo vya habari wajenge mazingira mazuri ya kuwawezesha
waandishi wa habari kusafiri ndani na hata nje ya nchi. Kwa kufanya
hivyo unawapa fursa nzuri ya kujifunza mambo mengi ya kuihabarisha jamii
ya Watanzania.
“Mwandishi
asiye safari anakuwa na uelewa finyu wa mambo kwani ni jambo la msingi
ajue nchi nyingine mambo yanaendaje ili aweze kulinganisha na maendeleo
ya nchi yetu,” alisema Kamuhanda.
Kamuhanda alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya habari kuwapa fursa waandishi wa habari kusafiri hilo ni jukumu lao la kwanza.
Kamuhanda
aliongeza kuwa hata yeye alipokuwa mwandishi wa habari alijifunza mambo
mengi alipokuwa akisafiri ndani na nje ya nchi, kwani kusafiri
kunapanua mawazo na kuwa na uwezo mpana “exposure” wa kupambanua mambo
juu ya nini cha kuandika na kuuhabarisha umma kulingana na maadili ya
uandishi wa habari.
Aidha,
Kamuhanda aliwaasa wamiliki na waadishi wa habari kuutumia vizuri uhuru
wa vyombo vya habari uliopo hapa nchini. Sanjari na hilo, aliviasa vile
vinavyokiuka miiko na maadili ya habari na kutumia vibaya uhuru huo
vitambue kuwa wote wapo kwa ajili ya kuiletea sifa nzuri nchi yetu.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara hiyo, Sihaba Nkinga
amempongeza Katibu Mkuu huyo aliyemaliza muda wake kwa kuitumikia Wizara
hiyo kwa uaminifu kwa kipindi cha wa miaka minne.
Sihaba
alisema kuwa Wizara anayoiongoza itaenzi kwa kusimamia na kuendeleza
mambo aliyoanzisha Kamuhanda ikiwemo kudumisha umoja wa watumishi katika
wizara na taasisi zake.
Naye
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Profesa Hermans Mwansoko akitoa neno
la shukrani kwa Kamuhanda kwa niaba ya wafanyakazi alisema wizara hiyo
itamkumbuka Kamuhanda kwa mpango wa kuwa na ofisi ya uhakika Dodoma,
kuanzisha Bodi ya Filamu, kujali afya na uzima wa watumishi na kujali
suala la jinsia katika ngazi za maamuzi ndani ya Wizara.
Kamuhanda
alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kufanya kazi chini ya Mawaziri
George Mkuchika, Naibu wake Joel Bendera, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Naibu
wake Fenella Mkangara.
Hadi
mabadiliko ya nafasi za makatibu wakuu yalipotokea hivi karibuni
alifanya kazi chini ya Waziri Fenella Mkangara Naibu wake akiwa Amos
Makala.
0 comments:
Post a Comment