Diwani
wa Kata ya Katuma Salvatori Msela mwenye shati la mikono mifupi
akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kapanga wakiwa na Diwani mwenzake wa
Kata ya Mpanda ndogo Mohamed Mapengo mwenye shati la mikono mirefu,
wakiongea na wananchi katika kujadili na kupanga mipango ya maendeleo na
kuwahimiza wananchi kujitolea nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa
Zahanati. Wananchi
wa Kijiji cha Kapanga wakimsikiliza Diwani wao katika moja ya mikutano
ya kuhamasisha uchangiaji wa shughuli za maendeleo Mheshimiwa Diwani
hayupo Pichani,Kijiji cha Kapanga kiko Kata ya Katuma Tarafa ya Mwese
kwenye nyanda za miunuko ya milima ya mwese, umbali wa zaidi ya
kilometa 75 kutoka Mpanda Mjini Mkoani KATAVI.
(Picha zote na Kibada Kibada Katavi)
Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi
Wakazi
wa Kijiji cha Kapanga kilichopoo Kata ya Katuma Tarafa ya Mwese Wilaya
ya Mpanda kinakabiliwa na ukosefu wa Huduma muhimu za kijamii hali
inayowafanya wananchi wa kijiji kuwahatarini kukubwa na magonjwa ya
mlipuko kutokana na kukosa huduma ya maji safi na salama..
Hayo
yalielezwa na Diwani wa Kata ya Katuma Salvatory Msela wakati akiongea
muda mfupi baada ya ziara kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Halmashuri katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Diwani
Msela alizitaja huduma zinazokikabili kijiji hicho ambazo ni muhimu na
wananchi wa Kijiji cha Kapanga wanazokosa kuwa ni huduma ya Maji safia
na salama.
Alieleza
kuwa wananchi wa kijiji hicho hawana huduma ya maji safi wala salama
,siyo maji ya bomba wala yale ya kisima na wanategemea maji
yanayotiririka kutoka kwenye vijito vilivyopo kijijini hapo maji amabayo
siyo rafiki kwa matumizi ya binadamu.
Huduma
nyingine wanayokabiliwa nayo ni ukosefu wa huduma ya Afya kwa kuwa
kijiji zahanati,badala yake wanategemea kununua dawa kutoka kwenye
vibanda vinavyouza bidhaa za kawaida wanauza vidonge aina ya panado
ili kutoa huduma kwa wananchi wakazi wa kijiji hicho.
Akifafanua
zaidi alieleza kuwa wananchi hao kutokana na ukosefu wa huduma muhimu
za Afya akiwa na maana zahanati na maji hali yao iko hatarini iwapo
kutatokea magonjwa ya mlipuko kama kuhara kwa kuwa wanatumia maji ambayo
siyo safi wala salama ni maji ya mto na asilimia kubwa ni maji
machafu kwa kuwa hata wanyama wanayatumia.
Kuhusu
huduma ya Afya wananchi wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya
kilometa kumi kufuata huduma ya tiba na wanaohangaika zaidi na akina
mama na watoto wa Kijiji cha Kapanga wanaoenda kufuata huduma Katuma
makao makuu ya Kata ilipojengwa zahanati.
Kufuatia
hali hiyo Diwani wa Kata ya Katumba aliomba Serkali kupitia Halmashauri
kuweka bajeti katika mipango ya maendeleo ya kuwasogezea huduma ya
Afya na Maji wananchi hao wa kijiji cha Kapanga ili nao waweze kujisikia
kuwa wanafaidi matunda ya nchi kama ilivyo kwa wananchi wenzao wa
maeneo mengine.
Akizungumzia
shule alieleza kuwa kwa upande wa shule walijitahidi kujenga madarasa
ambapo shule ina madarasa japo hayatoshelezi lakini angalau watoto
wanasoma tofauti na huduma ya Afya na Maji.
0 comments:
Post a Comment