Wafanyabiashara
Ambele Mwasyeba (kulia) na Sebastian Kavishe wanaotuhumiwa kuhujumu
Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits kwa kuuza bia ya Windhoek bila
ya kuwa na kibali cha kampuni hiyo wakisindikizwa na askari polisi
kuingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo
kusomewa mashtaka yao. Kampuni ya Mabibo ndiyo pekee iliyoruhusiwa
kisheria kuingiza na kusamabaza kinywaji hicho hapa nchini
Picha na Philemon Solomon wa Fullshangwe Dar es salaam
WAFANYABIASHARA
wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kuingilia
hakimiliki ya biashara.
Wafanyabiashara
hao wanadaiwa kuingilia haki miliki ya kibiashara ya kampuni ya Mabibo
Beer Wines and Spirits Limited ya jijini Dar es Salaam.
Washitakiwa
hao Ambere Mwasyeba (38) mkazi wa Mbezi Beach na Sebastian Kavishe (45)
mkazi wa Yombo kwa Abiola, walipandishwa kizimbani Mahakamani leo
Septemba 25-2013 na kusomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu MKazi Gene
Dudu.
Wakili
wa Serikali Charles Anindo aliwasomea washitakiwa hao mashitaka yao,
ambapo wanadaiwa kuingilia haki miliki ya kibiashara ya kampuni hiyo kwa
kufanya biashara ya katoni 1850 za bia aina ya Windhoek zenye thamani
ya Sh milioni 107.3.
Ilidaiwa
washitakiwa hao walifanya biashara hiyo bila kuwa na alama halali ya
MB66 iliyosajiliwa kwa kampuni hiyo, huku wakijua kufanya hivyo ni
kinyume cha sheria.
Hata
hivyo washitakiwa hao walikana mashitaka yao na kurudishwa rumande
baada ya kuzuka mvutano wa kisheria kati ya upande wa mashitaka na
upande wa utetezi juu ya dhamana ya washitakiwa. Ambapo upande wa
mashitaka ukitaka washitakiwa watoe dhamana ya hati ya mali
isiyohamishika ama kuwasilisha nusu ya fedha ya mali hiyo kwa mujibu wa
sheria sura ya 148 kipengele (5) kifungu kidogo (e).
Hata
hivyo kwa upande wa wakili wa utetezi , Living Kimaro alidai kuwa kosa
hilo si fedha kama mali, hivyo hakuna sababu ya wateja wake kutoa nusu
ya thamani ya mali hiyo.
Wakili
Anindo alidai kwa mujibu wa sheria haki yoyote iliyothibitishwa
kisheria ni mali. Hakimu Dudu aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapokuja
kwa ajili ya uamuzi wa dhamana.
0 comments:
Post a Comment