Dar
es Salaam. Wataalamu wa sekta ya pamba nchini, wamesema kama wakulima
wa pamba watasaidiwa kuendeleza kilimo cha mkataba kilimo hicho
kitabadilisha maisha yao.
Mkaguzi wa Pamba katika Wilaya
ya Bunda, Igore Manonga, alisema kuanzishwa kwa kilimo cha mkataba,
kumeleta faida kwa wakulima wa zao hilo na kwamba kuna haja ya
kukiendeleza.
“Kabla ya kuanzishwa kwa kilimo
cha mkataba, uzalishaji wa pamba wilayani Bunda ulikuwa wastani wa kilo
250 mpaka 300 kwa ekari, lakini baada ya kuanzishwa katika msimu wa
mwaka 2010 uzalishaji uliongezeka na kufikia kilo 300 hadi 600 kwa ekari
moja,” alisema Manonga.
Alisema baadhi ya wakulima wanazalisha hadi kilo 1,000 kwa ekari yakiwa ni matokeo ya kilimo cha mkataba.
Mkaguzi
wa Pamba wilayani Butiama, Alphone Ngewagale, alisema karibu kila
wilaya yenye mradi wa kilimo cha mkataba, uzalishaji wa zao hilo kwa
ekari umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment