Mwezeshaji
Liliani Timbuka kutoka( MCT) ambaye pia ni Mhariri Gazeti la Uhuru na
Mzalendo akiwasilisha mada kwa washiriki wa semina iliyohusu nanma ya
kulinda Waandishi Habari wakati wa kuandika habari maeneo yasiyo rafiki
waandishi hao hawapo
Waandishi
Wakijadiliana katika mara baada ya mtoa mada kuchokoza muda mfupi baada
ya kuwasilisha mada hapo wanatafakari kwa kupanga mbinu na mada nzito
nini kifanyike kuokoa maisha ya waandishi ambayo yanaelekea mlama
kutokana na zahama wanayokumbana nayo kila siku katika kazi zao za kila
siku kuhabarisha umma
Waandishi
Habari wa mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa na Ruvuma wakiwa nje ya
Hoteli ya Mbeya Paradise katika Picha ya Pamoja na wawezeshaji mara
baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili iliyohusu nanma ya
kujilinda wakatika wa kuandika habari maeneo hatarishi au maeneo
yasiyorafiki kama maeneo ya vita.
Na Kibada Kibada –Mbeya
Waandishi
Habari wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili taratibu na
Kanuni zinazotawala taalum ya Habari ili kuepusha migogoro inayoweza
kujitokeza katika jamii.
Rai
hiyo imetolewa na Beda Msimbe wakati akiwasilisha mada inayohusu
maadili ya uandishi Habari kwenye mafunzo ya siku mbili ya Waandishi
wa Habari katika maeneo hatarishi na jinsi gani ya waandishi
watakavyoweza kujilinda ili wasiweze kuzulika wakati wanatekeleza kazi
zao za uandishi wa Habari.
Akiwasilisha
Mada inayohusu maadili ya Uandishi wa Habari Mwezeshaji huyo kutoka
(MCT) ambaye pia ni Mwandishi Mkongwe katika Tasinia ya Habari hapa
Nchini ameeleza kuwa tatizo kubwa kwa waandishi wa sasa hawazingatii
madili ya Uandishi wanapokuwa wanafanyakazi za uandishi hali ambayo
inaleta migongano miongoni mwa jamii.
“Waandishi
kwanza niwavivu wa kusoma hawataki kujituma ili kuweza kufanya mambo
kwa uhakika tofauti na waandishi wa siku za nyuma na wengine miongoni
mwetu hao hao wanajifanya polisi, usalama wa taifa Uhamiaji hao hao
achana na mambo hayo fanya kazi yako ya uandishi kwa kufuata misingi ya
kazi yakomtakufa hatutaki maiti sisi tunataka ututlete habari maiti
hataweza kuongea naye wala hatoweza kutusaidia sisi”alisema Msibe.
Utaacha
familia inateseka bure watoto wako wazazi wako hao ndi
watakaohangaika,”Sisi tunapenda uishi tuona unaendelea kuishi hatupendi
mfe ndiyo maana tunakuja kuwapa mbinu za kujilinda,na ipo haja ya watu
kujiunga na mafunzo ya mgambo angalau muelewe jambo mbinu kidogo za
kujilinda kwa wale ambao hawakupita Jeshila kujenga Taifa JKT”aliongeza
kusema.
Mwezeshaji
huyo ameendelea kueleza kuwa kulingana na mazingira yaliyopo sasa
waandishi wamekuwa wahanga wa mashambulio ya kupigwa kumwagiwa
tindikali,kujeruhiwa na pengine kuuwawa kutokana na migongano
inayojitokeza .
Kutokana
na waandishi wenyewe wakati mwingine wanachangia wanapoandika habari
ambazo zinapendeea upande mmoja au zinazoegemea upande mmoja upande wa
pili unaonekana kama umeonewa inakuwa chanzo cha migogoro.
Naye
Liliani Timbuka akiwasilisha mada inayohusu jinsia na unyanyaswaji
unaofanyiwa wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu katika jamii
alieleza kuwa habari za wananwake na watoto zinaandikwa vibaya na kwa
wingi zaidi.
Timbuka
alfafanua kuwa tofauti na habari za watu wengine kama wanaume badala
ya kuuandikwa kwa uzuri unakuta ubaya zaidi ndio unaotawala katika
habari za jinsia fulani hasa wananawake hapo haki haitendeki yale mabaya
wanayofanyiwa ndiyo yanayoandikwa kwa wingi sana hali hiyo siyo zuri
kwa jamii inayohusika inajisikia kutotendewa haki.
Ameasa
wandishi wa Habari waisaidie jamii kwa kuandika mambo ambayo
yatasaidia kujenga na kuondoa matatizo katika jamii husika ili jamii
hiyo iweze kupata maendeleo.
Alieleza
kuwa Waandishi wa Habari ni watu muhimu sana wao ndio wanaoweza kujenga
nao wao hao hao ndio wanaoweza kubomoa hvyo ni wajibu wa waandishi
kufanya kazi zao kwa kuzingatia madili taratibu kanuni na sheria za
uandishi zinavyosema ili kueousha migogoro.
Kwa
upande wake Mshiriki wa semina hiyo kutoka Rukwa Nsima Ernest ambaye
alikuwa Mwenyekiti wa Semina hiyo alieleza kuwa waandishi wa Habari
wamekosa uzalendo ndiyo maana wanafanya mambo ambayo hayaendani na
taalamu waliyosomea wanatakiwa wajitume wajitoe wawe na uzalendo na nchi
na kile wanachikifanya,.
Aidha
ameleza kuwa wajitoe na watambue kuwe Dhaman ya ulinzi wake uko
mikononi mwake mwenye kwanza kabla ya mtu mwingine, kwanza watambue
hilo na wasijiingize katika masuala ya kisiasa wafanye mambo kulingana
na taaluma waliyonayo.
Ili
waandishi wa Habari waweze kwenda vizuri ni lazima warudi kwenye
misingi ya Uandishi wa Habari wazingatie 5Ws+H iwapo watafuata hayo
wataandika habari zenye ukweli, usahihi,zisizopendelea upande wowote na
hapo wataepusha migongano na kupunguza chuki na kupigwa kwa kuwa
watakuwa hawajapendelea upande wowote bali watakiwa wametenda haki.
Lakini
kwa wakati huu waandishi wa Habari wamekuwa sehemu ya ushabiki kwa
kuandika taarifa bila kuzifanyia utafiti matokeo yake ni kuchochea
migogoro katika jamii.
Semina
hiyo iliwashirikisha waandishi wa Habari kutoka Mikoa Minne ya Mbeya,
Rukwa, Katavi na Ruvuma, iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania
(MCT) kwa ajili ya kuwapatia Mafunzo na mbinu za kujilinda wakati
wakiwafanya kazi katika maeneo hatarishi kwa maisha yao kulingana na
hali ilivyo kwa sasa kulingana na mabadiliko na Mazingira yaliyopo kwa
sasa ambayo waandishi wengi wanauwawa kila kukicha kote dunia na
Tanzania ikiwemo.
0 comments:
Post a Comment