Wednesday, September 25, 2013

DSC_4998 
Ashanti United, Wazee wa kuchezea za uso ligi kuu soka Tanzania bara, toka ligi imeanza hawajaonja ushindi zaidi ya sare moja.

Na Baraka Mpenja , Mbeya
KWA mara nyingine huenda Ashanti United wakaendelaza rekodi yao mbaya ya kupanda na kushuka  katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara baada ya leo hii kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Rhino Rangers Uwanja wa A.H. Mwinyi mjini Tabora.
Mchezp huo pekee wa ligi kuu ulitarajiwa kuwa wa kufuta makosa kwa Ashanti kwani tangu waanze ligi kuu wamekuwa wakipokea kichapo kasoro tu mwishoni mwa wiki walipotoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam fc uwanja wa Azam  Complex uliopo maeneo ya Chamazi Mbande nje ya jiji la Dar es salaam.
Ashanti ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda ligi kuu na inaonekana kuwa daraja la kuchukulia pointi tafouti na timu za Mbeya City na Rhino ambazo kwa kiasi kikubwa zimeonesha soka safi na upinzani wa hali ya juu.
Kipigo cha leo kinawapa raha zaidi mashabiki wa Rhino waliokuwa na hamu ya kupata matokeo ya ushindi katika dimba lao la A.H. Mwinyi, lakini kwa upande wa mashabiki wa Ashanti mambo yanazidi kwenda kombo.
Baada ya kipigo cha leo, wauza mitumba hao wa Ilala jijini Dar es salaam, wanarejea katika uwanja wa nyumbani wa Azam Complex jumapili ya wiki hii kukabiliana na Mtibwa Sugar.
Kutokana na ubora wa Wana TamTam, Ashanti wanaweza kujikuta wakiambulia kipigo kingine na kuendelea kujichimbia mkiani mwa ligi hiyo.
Wao Rhino Rangers watakuwa kibaruani siku ya jumamosi (septemba 28) kukabiliana na vijana wa Kagera Sugar katika uwanja wao wa nyumbani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video