Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Vijana
nchini wametakiwa kuwa wawazi, waaminifu na waadilifu kwani huo ndiyo
msingi mkubwa wa kupambana na rushwa ili waweze kuwa viongozi wazuri
hapo baadaye.
Rai
hio imetolewa leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai
wakati akiongea na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Veta likichopo
katika Manispaa ya Lindi mara baada kuzindua klabu ya kupinga rushwa
chuoni hapo.
Alisema
kuwa hivi sasa kuna baadhi ya viongozi ambao wanakusanya mapato na kodi
za wananchi na kuzitumia vibaya na hivyo kusababisha shughuli za
maendelea kutofanyika ikiwa ni pamoja na kutojengwa kwa shule na vituo
vya afya na wanaoathirika ni wananchi wote.
Simai
alisema, “Vijana ni tegemeo la taifa chukueni hatua dhidi ya rushwa,
kila mtu awajibike kwa kutoa taarifa na ushahidi ili wahusika
wachukuliwe hatua ni lazima mjifunze kutokana na makosa yanayofanyika
leo ili nanyi msifikie huko kwani rushwa ni mbaya na adui mkubwa wa
maendeleo”
Kiongozi
huyo wa mbio za Mwenge Taifa alisema mtu ukiwa muadilifu na muaminifu
hata sehemu ya kazi utaonekana na utapanda kutoka hatua moja kwenda
nyingine bila ya kutoa rushwa na kutoa mfano kwa wanafunzi hao mara
baada ya kumaliza masomo yao watapata ajira bila ya kutoa rushwa kwani
ni haki yao kuajiriwa au kujiajiri.
“Kama
wananchi watapata taarifa na haki zao kwa wakati kutoka kwa viongozi
wao wataepukana na mazingira ya rushwa lakini hivi sasa kuna baadhi ya
watu wanaona kuwa hawawezi kupata haki zao za msingi hadi watoe rushwa.
Ninawaomba
wale wote wenye tabia hii muiache na mtoe taarifa kwa Taasisi ya
Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ili pale mnapoombwa kufanya hivyo
kwani rushwa ni adui wa haki na mfahamu kuwa kwa anayetoa na anayepokea
wote wanakabiliwa na kosa la jinai”, alisema Simai.
Simai
alisema kuwa ni muhimu vijana wakawajibika na kuwa wawazi katika mambo
wanayoyafanya kwa maana ya kwamba wakipata nafasi wawashirikishe na
wengine pia wafuate misingi ya utawala bora katika kupambana na rushwa.
Akisoma
taarifa ya klabu ya wapinga rushwa katika chuo hicho Christina Mkolela
ambaye ni mwanachama alisema kuwa ili kupambana na rushwa katika
halmashauri ya Manispaa ya Lindi waliamua kuanzisha klabu hiyo ikiwa ni
moja ya mkakati wa kuelimisha vijana waliopo vyuoni ili kuwajengea
uzalendo wa kuchukia rushwa na baadaye kuwa raia wema wasiopenda kupokea
wala kutoa rushwa.
Alisema
klabu hiyo ilianzishwa mwaka 2013 ikiwa na wanachama 91 kati ya hao
wasichana ni 21 na wavulana ni 70 ambao wanashiriki katika kutoa elimu
ya kuzuia na kupambaa na rushwa kwa wenzao.
Mkolela
alisema, “Klabu hii ni ya kudumu na itaendelea kupokea wanachama ambao
ni wanavyuo watakaokuja chuoni hapo kila mwaka na hivyo kuifanya kuwa
endelevu”.
Kabla
ya kuwasili chuoni hapo Mwenge huo wa uhuru ulipokelewa kutoka wilaya
ya Lindi na viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wa Manispaa ya
Lindi akiwemo mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika eneo la Mto Mkavu –
Mbanja.
Ukiwa
katika Manispaa ya Lindi Mwenge wa uhuru utafungua, kuzindua na kuweka
mawe ya msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi
bilioni 1.5 kati ya miradi hiyo ni mradi wa maji safi kwa matumizi ya
binadamu na mradi wa samaki.
Sherehe
za kilele za mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zitaenda sambamba na
kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na
maadhimisho ya wiki ya vijana zinatarajia kufanyika tarehe 14/10/2013
katika uwanja wa Samora uliopo Manispaa ya Iringa.
0 comments:
Post a Comment