Na Baraka Mpenja, Mbeya
HOMA
ya pambano la kukata na shoka baina ya wakali wanaotikisha soka la
bongo kwa sasa na kuwafanya mashabiki waumize vichwa juu ya ujio wake,
klabu ya Mbeya City dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union katika uwanja
wa sokoine jumamosi yazidi kupanda, huku mashabiki wa jiji la Mbeya
wakisubiri kuona timu yao ikiwacharaza bakora za moto wapinzani wao.
Kipute
hicho kinazidi kutawala katika midomo ya wapenda soka kutokana na ubora
wa timu zote mbili, hasa Mbeya City ambao siku za karibuni wamebadili
sura ya ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuonesha upinzani mkali
zaidi kwa vigogo Yanga na Simba.
Klabu
hii ambayo wachezaji wake hulipwa mishahara na Halmashauri ya jiji,
iliibana Yanga Uwanja wa sokoine na kutoka sare ya bao 1-1, huku Yanga
wakilalamikia kufanyiwa vurugu na kukata rufaa wakidai mechi ichezwe
upya katika uwanja mwingine.
Hapa
vijana wa Mbeya City walikuwa wanamuomba Mungu wao kabla ya kuanza
kibarua dhidi ya Simba jumamosi ya wiki iliyopita jijini Dar es salaam
Lakini
kutokana na kiwango cha Mbeya City watu wengi wanaamini kuwa Yanga
walikuwa wanajisafisha mbele ya mashabiki wao kwani walibanwa dakika
zote na kukoswa koshwa dakika za lala salama na kama wangezembea hadidhi
ingekuwa nyingine.
City
waliwashangaza wengi zaidi walipotia maguu yao kwa mara ya kwanza
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Vinara Simba Sc jumamosi
ya wiki iliyopita na kutoka sare ya mabao 2-2.
Vijana
Walipiga soka la hatari na kuugeuza uwanja mzima kuwa burudani kubwa ya
soka, huku mashabiki wengi wakilipuka kwa kushangilia soka maridhawa la
vijana hawa na kupelekea mashabiki wa Simba kuomba mpira uishe kwani
hali ilikuwa tete na kama zingeongezwa dakika chache, furaha ingeingia
shubiri.
Wazee wa Mzuka wanaisubiri mechi ya jumamosi dhidi ya Coatal Union uwanja wa sokoine jijini Mbeya
Kuelekea
mchezo wa mwishoni mwa wiki, kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema
maandalizi yanaendelea kama kawaida, lakini wao walishajiandaa siku
nyingi na sasa kazi yao ni kujiweka sawa kwa kila mechi.
“Tulijiandaa
sana kabla ya ligi kuanza, mashindano yameanza, kwa sasa tunatekeleza
mipango yetu. Vijana wanashika mafunzo, wapo katika morali kubwa na
tunawataka kuongeza bidii zaidi. Tunawaheshimu Coastal, lakini
tutakabiliana nao kwa lengo la kusaka ushindi”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi
aliyejizolea umaarufu na kuwa gumzo kubwa nchini kwa sasa, aliongeza
kuwa kwa sasa wamerejea nyumbani baada ya mechi mbili za ugenini ambapo
wameambulia pointi 2, kwahiyo mipango yao ni kshinda mechi hiyo muhimu
kwao na kujikusania pointi zote tatu kwa mara ya pili tangu kuanza kwa
mitanange hiyo.
Aidha
aliwataka mashabiki wa soka jijini Mbeya kujitokeza kwa wingi
kuwashangilia vijana wao wenye uchu wa kupata matokeo mazuri na kubadili
sura ya soka la Tanzania linalotawaliwa na klabu kongwe za Simba na
Yanga.
Kikosi cha Wagosi wa Kaya
Wakati
huo huo, jumapili ya wiki hii, Uwanja wa sokoine utahimili daluga za
wanaume wawili, Tanzania Prisons “Wajelajela” dhidi ya makamu bingwa wa
ligi kuu , Azam fc wenye kumbukumbu ya kuilaza Yanga kwa risasi 3-2
jumapili uwanja wa Taifa.
Prisons
wataingia Uwanjani kusaka ushindi wa kwanza baada ya kufungwa mechi
mbili za kwanza, na kutoka sare mechi tatu dhidi ya Coastal Union uwanja
wa Mkwakwani, Yanga na Mtibwa Sugar katika uwanja wao wa Sokoine.
Mechi
nyigine za jumamosi (Septemba 28) ni kama ifuatavyo; Yanga vs Ruvu
Shooting, Uwanja wa Taifa, Rhino Rangers vs Kagera Sugar, A.H. Mwinyi,
na Mgambo JKT Vs JKT Oljoro, Mkwakwani Tanga.
Jumapili
(septemba 29 ), JKT Ruvu watakwaruzana na Wekundu wa Msimbazi Simba
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Vibonde Ashanti United watakuwa
Azam Complex kuvaana na Mtibwa Sugar, wakati Prisons watakuwa Sokoine
kukabiliana na Azam fc.
0 comments:
Post a Comment