Serikali imefuta vibali vya kuingiza kemikali nchini. |
Serikali
imefuta vibali vya kuingiza kemikali nchini ikiwa ni moja ya hatua za
kudhibiti matumizi ya kiuhalifu na kutishia maisha ya wananchi.
Aidha, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuwapo kwa matukio ya mara kwa mara kwa wananchi kumwagiwa tindikali.Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, alitangaza hatua hiyo juzi wakati akizungumza na Dawati la Mkoa la Ukatili wa Kijinsia ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa katika warsha iliyolenga kutoa elimu juu ya umuhimu wa kumtumia Mkemia Mkuu.
Profesa Manyele alisema kuwa serikali inaendelea kupambana na uingizaji holela wa kemikali ambao ndiyo chanzo cha kubadili matumizi yake na kuangamiza maisha ya wananchi.
Alisema kuwa tatizo kubwa walilolipata ni kutokana na waingizaji, wasafirishaji, watumiaji kubadili matumizi ya kemikali hizo na kuzifanya sehemu ya silaha za kuangamiza wananchi.
Profesa Manyele ambaye yupo katika ziara ya siku sita mkoani, alisema kuanzia sasa wanaohitaji vibali hivyo watalazimika kuomba upya.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment