Na Baraka Mpenja, Mbeya
“MTU
akifanya jambo jema, kumpongeza ni haki yake”, leo hii mtandao huu
umepata nafasi ya kutembelea uwanja wa kumbukumbu ya hayati Edward
Moringe Sokoine jijini hapa na kujionea namna shughuli za ukarabati wa
uwanja zinavyoendelea kabla ya mechi kali ya kukata na shoka baina ya
wenyeji Mbeya City dhidi ya mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara,
klabu ya Yanga ya Dar es salaam.
Kwasasa
uzio wa uwanja huo unaotenganisha wachezaji wakiwa uwanjani na
mashabiki wa majukwaani unaimarishwa pamoja na dimba lenyewe kuwekwa
sawa, na mpaka sasa wapo hatua za mwisho kuzungushia uwanja mzima.
Hakika
ni mabadiliko makubwa sana na uzio huu ni mrefu na wakutosha, waya
zote ni mpya, na hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuwazuia mashabiki
kuingia uwanjani baada ya mechi, labda maaskari wazembee.
Siku
za nyuma, uzio wa uwanja huu ulikuwa mbaya sana na ilikuwa ngumu sana
kuwazuia mashabiki wenye mdadi mkubwa na soka kuingia uwanjani baada ya
mechi na kushangilia, hali ambayo ilikuwa hatari sana kwa wachezaji,
viongozi wa timu na waandishi wa habari wanaokuwepo kufanya shughuli zao
wakati wa mechi.
Lakini
kwa sasa hali itakuwa shwari na pongezi kubwa ziwaandee wamiliki wa
uwanja, Chama cha Mapinduzi CCM ambapo Meneja Modestus Mwaluka ndiye
mwenye dhamana kusimamia uwanja huo.
Wakati
huo huo, leo hii chama cha soka jijini Mbeya, MREFA kimetangaza vituo
vya uuzaji wa tiketi jijini hapa na baadhi ya vituo hivyo ni Ilomba,
Uyole, Iyunga, Kabwe, sokoine uwanjani n.k.
Katibu
mkuu wa MREFA, Seleman Haroub amesema kiingiliao katika mchezo huo ni
Tsh.5,000/= na amewatahadharisha watu kununua tiketi maeneo ambayo si
maalumu kwani kuna watu wanaweza kuuza tiketi bandia.
“Tunajua
wazi kuwa watu wanajipanga kupiga pesa kwenye hii mechi, kwanza
tumejipanga kuzuia tiketi bandia kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Kiukweli mtu atakayekamatwa na tiketi bandia atakuwa amejitia kwenyae
matatizo makubwa sana na atafikishwa mamlaka zinazohusika”. Alisema
Haroub.
Haroub
amewaonya watu wanaotarajia kutumia mchezo huo kujipatia pesa kwani
ulinzi utaimarishwa kila kona na haki itatendeka kwa wale wote
wanaofuata taratibu za uwanjani, na wale wakaidi basi rungu
litawaangukia.
Katibu
huyo amesema mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa mkuu wa
mkoa wa Mbeya, Abas Kandoro na mpaka sasa wanaendelea kuwasiliana na
ofisi ya mkuu wa mkoa na hapo kesho watakuwa na kikao ambapo taarifa
rasmi itatolewa.
Hata
hivyo, Haroub amewaomba wakazi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi kushuhudia
mechi hiyo na kuishangilia Mbeya City kwani ni timu ya wananchi wote.
0 comments:
Post a Comment