Timu
ya mpira wa pete ya Utumishi ikiwa katika mazoezi kabla ya kupambana na
timu ya Wizara ya Mifugo.Utumishi iliishinda kwa maba 28-15
Timu ya Wizara ya Mifugo kabla ya kuanza mechi kati yake na timu ta Utumishi katika viwanja vya UDOM mjini Dodoma
Timu ya mpira wa pete ya Utumishi kabla ya kuanza kwa mechi kati yake na Wizara ya Mifugo katika viwanja vya UDOM mjini Dodoma..
Timu ya mpira wa pete ya Utumishi ikisalimiana na timu ya Mifugo kabla ya mechi kuanza katika viwanja vya UDOM.
Timu ya Utumishi ikimenyana na timu ya Mifugo katika viwanja vya UDOM mjini Dodoma jana jioni.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Timu
ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
imeendeleza ubabe katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendela katika
viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma baada ya kuichakaza timu ya Mifugo kwa
magoli 28 kwa 15 jana jioni.
Mchezo
huo ulioanza kwa kasi huku kila timu ikimsoma mpinzani wake hata hivyo
Mifugo ilipelekwa kasi na Utumishi kwa kukubali magoli 16 kwa 6 hadi
kipindi cha kwanza kinamalizika. Katika kipindi cha kwanza Mifugo
walipoteza pasi 10 kwa kudhibitiwa na Monica Aloyce (GK) na Amina Ahmed
(WD) wa Utumishi.
Kipindi
cha pili kwa kiasi kikubwa kilimilikiwa na Utumishi hali iliyowafanya
wachezaji wa Mifugo kucheza ndivyo sivyo. Mchezo wa rafu ulisababishwa
mechi hiyo kusimamishwa mara kadhaa ambapo Fatma Ahmed (GS) na Secela
Shabani (WA) wote wa Utumishi kuumizwa. Katika kipindi hicho Utumishi
ilijiongezea magoli 12 na Mifugo kuambulia 9.
Baada
ya mchezo huo Kocha wa timu ya Utumishi Bw. Mathew Kambona alisema
mechi ilikua nzuri licha ya wachezaji wake kuumizwa kutokana na mchezo
wa rafu.
“Tunajipanga vizuri ili kuhakikisha wachezaji walioumizwa wanakuwa sawa kwa michezo inayokuja” Kambona alisema.
Hata hivyo, kocha wa Mifugo Bi. Nora Nchuwekeleze alisema bado anaamini timu yake ni nzuri.
Nchukuwekeleze alisema mchezo ulikuwa mzuri na wenye wenye ushindani.
Mwanamkasi
Abbasi (GK) anayeichezea Mifugo alisema walizidiwa kutokana na
wachezaji watatu tegemeo kuwa majeruhi hivyo kuzidiwa mbinu na maarifa
na wapinzani wetu.
Timu
ya Utumishi itaingia katika mzunguko wa pili wa Michezo ya SHIMIWI kwa
upande wa mpira wa Pete baada ya kupatikana kwa mshindi katika mchezo
kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Katiba na Sheria
mechi itakayochezwa leo jioni.
0 comments:
Post a Comment