Na Eleuteri Mangi- Maelezo
SERIKALI
ya Tanzania na Uswisi zimetiliana mkataba makubaliano wa kuisaidia
mpango wa taifa wa kupambana na malaria nchini (NMCP) nchini wenye
thamani ya Sh. bilioni 10.3.
Mkataba
huo wa makubaliano hayo umetiwa saini leo jijini Dar es Salaam na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Dkt. Servancius Likwalile na
Balozi wa Uswisi nchini Olivier Chave.
“Nimefurahi
kubainisha kuwa lengo kuu la kutia saini makubaliano ya msaada huu ni
kupunguza vifo vya watoto na akinamama vinavyosababishwa na ugonjwa wa
malaria hasa makundi hayo hatarishi kwa kuimarisha na kusaidia NMCP,”
alisema Dkt. Likwalile.
Dkt.
Likwalile alisema kuwa Serikali ya Tanzania inaichukulia Serikali ya
Uswisi kuwa ni moja kati ya rafiki waaminifu katika masuala ya
maendeleo.
Alisema
kwa takwimu za hivi karibuni, matokeo yanaonesha kuwa kumekuwa na
maboresho mazuri hasa katika kuzuia malaria kwa watoto chini ya umri wa
miezi sita hadi 59 vimepungua zaidi ya nusu kutoka asilimia 18 mwaka
2007 hadi asilimia 10 mwaka 2012.
Aidha
Dkt. Likwalile alisema kuwa kumekuwa na maendeleo mazuri ya kupambana
na ugonjwa wa malaria licha ya changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta
ya afya.
Changamoto
hizo ni pamoja na ukweli kwamba kwa upande wa Tanzania Bara, ugonjwa wa
malaria bado ni tatizo kubwa linalowasumbaua Watanzania walio wengi
ambapo zaidi ya asilimia 93 bado wanaishi katika mazingira hatarishi ya
uwezekanao wa kuambukizwa ugonjwa huo.
Aliongeza
kuwa madhara yanayotokana na ugonjwa huo yanaiathiri jamii katika sekta
mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu ambapo wanafunzi hushindwa kumudu
masomo hasa wanapokuwa.wagonjwa.
Pia
wafanyakazi na wakulima wanapougua hushindwa kutekeleza majukumu yao.
Hivyo kupelekea familia na jamii kushindwa kuendesha maisha yao ya kila
siku.
Kwa
upande wake Balozi wa Chave alisema kuwa matokeo yanaonesha Tanzania
inafanya vizuri katika kupunguza ugonjwa wa malaria ambapo takribani
asilimia 91 ya wakazi wanatumia vyandarua, asilimia 72 ya watoto chini
ya miaka mitano na asilimia 74 ya wanawake wajawazito hulala katika
vyandarua vilivyowekwa dawa ya kuzuia mbu.
“Lengo
la mradi ni kusaidia NMCP katika kuzuia kuudhibiti na kutibu ugonjwa wa
malaria hasa katika kusimamia, kupima na kutoa dawa za malaria kwa
ufanisi mkubwa,” alisema Chave.
Balozi
Chave alisema kuwa mradi huo unaofadhiliwa na nchi yake umekuwa na
mafanikio makubwa ambapo takribani asilimia 48 ya vifo vya watoto wa
umri wa chini ya miaka mitano vimepungua kati ya mwaka 2000 hadi 2010.
Kwa
mantiki hiyo Balozi Chave alisema kuwa Tanzania inaweza kufikia malengo
ya millennia namba nne ifikapo 2015 ambapo ni nchi chache za Afrika
zinaweza kufikia malengo hayo.
Naye
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando
alithibitisha kuwa wizara yake itasimamia fedha hizo kulingana na
malengo yaliyokusudiwa.
Ushirikiano
huo wa maendeleo baina ya nchi hizo ulianza kati ya miaka ya 1960
uliolenga katika kudhibiti malaria wilaya ya Ifakara mkoa wa Morogoro na
mwaka 1981 serikali hiyo kupitia Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC)
lilijikita katika utoaji huduma za afya kwa lengo la kuendeleza
upatikanaji wa huduma bora za kiafya maeneo ya vijijini.
0 comments:
Post a Comment