Sunday, September 1, 2013


tff_LOGO19Na Boniface Wambura, TFF
Usaili wa waombaji uteuzi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) unaendelea na unatarajia kukamilika leo (Septemba 1 mwaka huu).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni ilianza usaili juzi (Agosti 30 mwaka huu) ambapo matokeo ya usaili yanatarajiwa kutangazwa keshokutwa (Septemba 3 mwaka huu).
Kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF itawasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi na kamati hiyo.
Vilevile kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ni kipindi cha kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya maadili. Kwa watakaokata rufani wanatakiwa kuambatanisha na ada ya rufani kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Septemba 6 mwaka huu.
KIUNGO WA SIMBA AONGEZWA TAIFA STARS
Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza mchezaji huyo ili kuimarisha sehemu ya kiungo. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video