Saturday, September 28, 2013

miss tz 
Na Jackson Kalikumtima
Mchakato wa kutafuta Washiriki wa Kambi ya Tanzania Top Model ulioanza wiki mbili zilizopita unaendelea mwishoni mwa wiki hii hapa jijini Arusha na Mjini Moshi.
Wasichana 20 watakaochaguliwa kutoka maeneo mbalimbali nchini ndio watakaounda kambi ya Taifa ambayo itaendeshwa kama Tamthilia halisi kwenye kituo kimojawapo cha Televisheni ambacho hakijatangazwa.
Leo Jumamosi katika ukumbi wa Mango Tree, Warembo wapatao 25 wako kwenye mchuano mkali wa kuwania nafasi mojawapo kati ya hizo ili waweze kuwakilisha jiji la Arusha katika mashindano ya Tanzania Top Model yanayotazamiwa kufanyia mwishoni mwa mwaka katika Jiji la Dar es salaam.
Kesho Jumapili, kinyanganyiro hicho kitahamia katika mji wa Moshi kwenye ukumbi wa Kilimanjaro Crane Hotel ambapo wasichana wa mkoa wa Kilimanjaro watakuwa wanakabiliana na Majaji watano wanaoendesha zoezi hili.
Wasichana waliokwisha chaguliwa ambao wataingia kwenye kinyanganyiro cha Tanzania Top Model ni kumi ambapo watatu wanatoka Mwanza, Mmoja Tarime na sita kutoka jiji la Dar es salaam.
Waliokwisha chaguliwa ni Neema Charles,Christna Christopher,Judith Materegu,Mariam Joseph, Zulfar Bundalah, Darline Mmari, Nuru Mfaume, Lorrain Clement, Elizabeth Boniface na Irene Kasanda.
Wiki ijayo, Auditiond zitahamia mkoani Dodoma ambapo tunategemea kupata washiriki zaidi.
Mashindano ya Tanzania Top model yatakuwa yanafanyika kwa mara ya kwanza nchini na mshindi wake atawakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Top Model of the World yaliyopangwa kufanyika nchini Ujerumani au Misri mapema mwakani.
Shindano la Tanzania Top Model ni zaidi ya shindano  la kawaida la uanamitindo, maana litashindanisha Mabinti wenye ndoto ya kuwa Wanamitindo wa Kitaifa na Kimataifa, litawajenga na kuwafanya wajiamini zaidi pia litawapatia fursa ya kushiriki kwenye mashindano na maonyesho ya mavazi mbali mbali ya Kimataifa.
Mashindano ya uanamitindo yaliyowahi kufanyika huko nyuma yalifanikisha wanamitindo wa Tanzania kuwa Models wa ngazi za ulimwengu na kupata fursa ya kutangaza urithi na utajiri wa nchi yetu katika Nyanja mbalimbali kimataifa. Hivyo tumeona kuanzisha Shindano hili ili liwe kichocheo kingine cha kuitangaza nchi yetu katika mavazi na sanaa nyingine kimataifa na kuwa chimbuko la nyota nyingine katika dunia ya Wanamitindo.
Mashindano ya kumtafuta Tanzania Top Model si mashindano ya kawaida kama tulivyo zoea mashindano ya kuwakutanisha Washiriki na kupima Mshiriki aliye bora tu kuliko wenzake, bali ni Mashindano ya kumtafuta Mwanamitindo bora wa Mfano.
Haya ni mashindano yatakayo ruhusu Jamii/ Wananchi/ Wadau kushiriki kuchagua mshindi kwa kiwango fulani na kuleta taswira ya kuwa Msichana atakaye bahatika kushinda atakuwa ni chaguo na mwakilishi wao wa kikweli kwenye mashindano ya kumtafuta Top Model of the World.
Imetolewa Arusha
28/9/2013

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video