JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
|
|
|
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua Pepe: [email protected]
|
Dar es Salaam
Septemba 19,2013
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Julai 29, 2013 aliagiza kufanyika kwa opereheni maalum ya kuondoa
uhalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita mbao kwa kiasi kikubwa
umechangiwa na kuwepo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.
Operesheni
Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi imeanza rasmi
Septemba 6, 2013 baada ya kutoa muda wawiki mbili kwa wahamiaji
wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari yao au
kuhalalisha ukaazi wao nchini.
Wakati
Operesheni hii ikifikia katika Wiki yake ya Pili, Serikali kupitia
kiongozi wa Operesheni Brigedia Jenerali Mathew Sukambi inawapongeza
watendaji wote wa operesheni hii kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa
unyenyekevu na kiuzalendo kuhakikisha kuwa zoezi la kuondoa uhalifu na
kukamata wahamiaji haramu linafanyika kwa nidhamu ya hali ya juu na
mafanikio.
Aidha, kumekuwepo na tuhuma mbali mbali zinazotolewa kupitia Vyombo vya Habari ambazo hazina ukweli.
Tuhuma za rushwa dhidi ya watendaji wa Operesheni Kimbunga
Operesheni
Kimbunga inahusisha watendaji kutoka vyombo mbali mbali nchini vikiwemo
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Idara ya Uhamiaji, Jeshi la
Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU), Idara ya
Usalama wa Taifa, Idara ya wanyamapori na taasisi nyingine za serikali.
Mazingira
ya kazi ya kuwakamata wahamiaji haramu na kuwahoji ili kuthibitisha
uraia wao ni ya wazi hayawezi kuruhusu watendaji kuweza kupokea rushwa
kama ilivyoripotiwa na Gazeti moja hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo
ni ukiukwaji wa sheria.
Hata
hivyo, wananchi wanapaswa kufahamu kuwa iwapo kuna mtendaji wa
operesheni hii ameomba na kupokea rushwa wanakiuka sheria, hivyo ni
vyema kama kuna mtu mwenye ushahidi wowote atoe taarifa kwenye ofisi za
TAKUKURU zilizopo mikoani na Wilaya zote nchini.
Zoezi la Operesheni Kimbunga halilengi kunyanyasa wazee, watoto na wanawake wasio Raia walioolewa na Watanzania
Operesheni
Kimbunga haikulenga kuwanyanyasa Wazee, Wanawake walioolewa na watoto
wao wadogo wanaoishi nchini bila kufuata Sheria ya uhamiaji.
Kuna
waliokuwa Wakimbizi 36,000 kutoka nchi ya Rwanda walioingia nchini
miaka ya 1959 hadi 1961 waliokuwa wakiishi katika mkoa wa Kagera katika
maeneo ya Kimuli, Nkwenda, Mwase na maeneo mengine ambao walipewa uraia
wa Tanzania kwa tajinisi mwaka 1983 isipokuwa watoto wao kwa kuwa wazazi
wao hawakuwaombea uraia huo. Raia hao 36,000 waliopewa uraia wa
tajinisi hawakuguswa na operesheni hii kwani ni watanzania isipokuwa
watoto wao ambao hawakuombewa uraia na wanaishi nchini bila hadhi yeyote
ya kiuhamiaji.
Pia
kuna raia wa kigeni waliokuwa wanaishi bila kufuata sheria za uhamiaji
na Uraia ambao zamani walikuwa wakimbizi lakini hadhi ya ukimbizi
iliondolewa baada ya nchi zao kuwa salama na kutakiwa kurudi.
Hata
hivyo, kama mheshimiwa Rais, Jakaya Mrisho Kikwete alivyoagiza kuwa
zoezi lifanyike likiwa na sura ya kibinaadam pale inapobidi, raia hao wa
kigeni waliokuwa wanaishi nchini bila kufuata sheria hususan wazee
wameruhusiwa kubaki na kusaidiwa kufuata taratibu ili kuhalalisha ukaazi
wao.
Aidha,
ieleweke kuwa kuzaliwa Tanzania pekee hakumpi mtu haki ya kuwa Raia
moja kwa moja mpaka taratibu nyingine zifuatwe. Kuna watoto walizaliwa
Tanzania na Raia wa nchi za nje waliokuwa wanaishi nchini kabla ya
kupatiwa uraia. Hao hawawezi kuwa raia moja kwa moja mpaka taratibu za
kisheria zifuatwe.
Aidha, Operesheni Kimbunga haikulenga kuvunja ndoa na kusambaratisha familia. Lengo ni kuondoa wahamiaji haramu.
Wanawake
walioolewa na Watanzania wametakiwa kujiorodhesha ili kupatiwa
utaratibu wa ukaaji wao. Wanaume walifunga ndoa na Watanzania
wanatakiwa kurudi katika nchi zao na wake na watoto wao na kwa wanaotaka
kuishi nchini wanatakiwa kuomba vibali vya kuishi kwa kufuata sheria na
taratibu za uhamiaji.
Taarifa
hii imetolewa na Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa Timu ya Habari na
Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Septemba 20,2013, Biharamulo,
Kagera. Kwa maelezo zaidi Email: [email protected].
0 comments:
Post a Comment