Timu ya mpira wa pete ya Utumishi ikipasha kabla ya kuanza mechi kati yake na RAS Manyara katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma.
Timu
ya mpira wa pete ya utumishi ikiwa tayari kwa ajili ya ukaguzi kabla ya
kuanza mechi kati yake na RAS Manyara katika viwanja vya Chuo Kikuu
Dodoma.
Timu
ya mpira wa pete ya RAS Manyara ikiwa tayari kwa ajili ya ukaguzi kabla
ya kuanza mechi kati yake na Utumishi katika viwanja vya Chuo Kikuu
Dodoma.
Mechi kati ya timu ya mpira wa pete ya Utumishi na RAS Manyara iliyofanyika viwanya vya Chuo Kikuu Dodoma. Mechi kati ya timu ya mpira wa pete ya Utumishi na RAS Manyara iliyofanyika viwanya vya Chuo Kikuu Dodoma.
Na Mwandishi wetu
Timu
ya mpira wa pete ya Utumishi imeanza vizuri mzunguko wa kwanza wa
mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) baada ya kuifunga timu ya mpira wa pete ya Mkoa wa
Manyara(RAS Manyara) mabao 36-8 katika viwanja vya Chuo Kikuu
Dodoma(UDOM) leo mchana.
Katika
mchezo huo, RAS Manyara ilianza kwa kasi kwa kumtumia mfungaji wake
Maua Shabani (GS) aliyefunga mabao 3 kabla ya Utumishi kuanza kuumiliki
mchezo huo kwa kutumia wafungaji wake Fatma Ahmed (GS) na Anna Msulwa
(GA) walioshirikiana na hatimaye kuiwezesha Utumishi kuongoza kwa mabao
18-4 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi
cha pili cha mchezo kiliongozwa na Timu ya Utumishi iliyoweza kuwatumia
wachezaji wake mahiri Amina Ahmed (GD), Elizabeth Fusi (C),Monica
Aloyce (GK) wakishirikiana na wafungaji wake na kuipatia Utumishi mabao
18-4 .Mpaka mchezo unamalizika Utumishi iliibuka mshindi kwa mabao 36-8
dhidi ya RAS Manyara.
Akiongea
mara baada ya mchezo huo kocha wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi
Bw.Mathew Kambona alisema timu yake haikucheza katika kiwango
kinachotakiwa kwa kuwa wapinzani walikuwa wanapewa nafasi ya
kushambulia.
“Pamoja
na kupata ushindi huu lakini timu yangu haikucheza katika kiwango
kinachotakiwa hivyo inatakiwa ifanye juhudi zaidi kucheza katika kiwango
cha juu” alisema Bw.Kambona.
Bw.Kambona
aliongeza kuwa timu ya Utumishi ingepata mabao mengi zaidi lakini
kutokana na makosa ya kiufundi maadui wamepata nafasi ya kuifunga timu
hiyo.
Naye
Katibu wa mpira wa pete wa RAS Manyara Bi.Flora Mollel alisema timu
yake imeshindwa kuchukua ubingwa kutokana na uchovu wa safari.
Alisema,timu hiyo imejipanga vizuri kwa mashindano yajayo hivyo timu nyingine zitegemee maajabu ya RAS Manyara kuanzia leo.
Katika hatua nyingine timu ya Utumishi inatarajia kucheza na timu ya Wizara ya Ujenzi Jumatatu ya Septemba 22 mwaka huu.
Mechi
kati ya Utumishi na RAS Manyara ni kati ya mechi zilizo kwenye mzunguko
wa awali kabisa wa mashindano ya SHIMIWI wa kuchagua timu zitakazoingia
robo fainali baada ya kupata washindi katika makundi tofauti tofauti.
0 comments:
Post a Comment