Mkuu
wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi kushoto na dereva wa kampuni ya Tasia
Hogistic ya jijini Dar es Salaam, Verry Philiph (39) wakikabidhiwa
cheti baada ya kupimwa shinikizo la damu na wateknolojia wa maabara wa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Theodol Babwanga kushoto na
Daniel Mwita wakati mkuu huyo alipozindua mpango wa upimaji wa afya kwa
madereva wa malori makubwa katika mizani ya Mikese kufuatia kampuni ya
TBL kuendesha zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wa malori ikiwa
kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikibeba
ujumbe wa “usalama unaanza kwangu kisha kwako na sisi sote” mkoani
Morogoro.Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL.
Steve Kilindo.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Chalinze, Innocent Sule akiwa anazungumzana
baadhi ya madereva wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya mikoa ya
Dar es Salaam na Arusha zoezi lililofanyika katika mizani ya Kiangaiko
iliyoko Msata Bagamoyo. Kampuni ya Bia Tanzania TBL, sh mil. 13 kwa
uongozi wa Hospitali Teule ya Tumbi kwa lengo la kufanikisha kupima
madereva wanaotarajiwa kufikia 800 ikiwa na lengo la kupunguza kama si
kumaliza ajali.
Mmoja wa madereva akichukuliwa vipimo na daktari |
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi kushoto na dereva wa kampuni ya
Tasia Hogistic ya jijini Dar es Salaam, Verry Philiph (39) kulia
wakipimwa shinikizo la damu na wateknolojia wa maabara wa hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Morogoro, Theodol Babwanga kushoto na Daniel Mwita
wakati mkuu huyo alipozindua mpango wa upimaji wa afya kwa madereva wa
malori makubwa katika mizani ya Mikese kufuatia kampuni ya TBL kuendesha
zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wamalori ikiwa kuanza kwa
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikibeba ujumbe wa
“usalama unaanza kwangu kisha kwako na sisi sote” mkoani Morogoro. Wa
tatu kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL. Steve Kilindo.
MKUU
wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ahmed Kipozi (kulia) akizungumza na
mmoja wa Daktari wakati alipokwenda kushuhudia zoezi la upimaji afya
kwa madereva, makondakta na watu mbalimbali kwenye siku ya kwanza ya
wiki ya nenda kwa usalama ambayo imefanyika katika mizani ya Kiangaiko
iliyoko maeneo ya Msata Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.Katikati ni
Meneja Uhusiano wa TBL,Doris Malulu.
0 comments:
Post a Comment