Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya bonanza la waandishi wa habari lililofanyika kwenye uwanja wa
General Tyre, Arusha. Unaweza
ukadhani kuwa ni wachezaji wa Azam FC, lakini hao ni kikosi cha kwanza
cha ‘mauaji’ cha timu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini Taswa SC
wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupambana na timu ya Radio
5. Katika Mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya General tyre mkoni
Arusha, Taswa SC ilishinda kwa mabao 3-1. Mchezaji
wa timu ya Taswa SC, Juma Pinto akituliza mpira uku akilindwa na
mchezaji wa Triple A. katika mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya
General Tyre, mkoani Arusha, Taswa SC ilishinda kwa mabao 3-1. Wachezaji
wa timu ya Taswa SC wakipasha moto mwili kabla ya kuingia uwanjani
katika uwanja wa General Tyre mkoani Arusha Jumapili. Taswa SC ilicheza
fainali na timu ya chuo cha uandishi wa habari cha Arusha (AJTC) na
kushindwa kufungana katika mchezo wa fainali. Hata hivyo timu hizo
zilishindwa kupigiana penati kutokana na giza na hivyo kugawana zawadi
ya mshindi wa kwanza.
……………..
Mwandishi Wetu, Arusha
Timu
ya Mpira wa pete (netball) ya wanahabari wa jijini Dar es Salaam,Taswa
Queen juzi ilitwaa ushindi katika bonanza la nane la Waandishi mkoa wa
Arusha, baada ya kuichapa timu ya chuo cha uandishi wa habari Arusha
Arusha(AJTC) magoli 21-1.
Wakati
Taswa Queen walikitwaa ubingwa kaka zao, TASWA SC , walishindwa
kunyakuwa kombe, baada ya kutoka suluhu na timu ya AJTC katika mchezo
mkali wa fainali, ambao ulisitishwa kutoka na kiza wakati wa mikwaju ya
penati timu hizo, zikiwa zimefungana 1-1.
Kutokana
na matokeo hayo, Meneja wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL),
Endrew Warden alikabidhi Mwenyekiti wa Taswa SC Majuto Omar fedha
taslim 200,000 na meneja wa AJTC Modaha Lucas alikabidhiwa kiasi cha sh
200,000.
Taswa
SC, walifanikiwa kuingia fainali baada ya kuichapa timu ya Radio 5
magoli 3-1 na baadaye kuifungua timu ya Arusha 1-0 katika mchezo mkali
wa nusu fainali.
Kwa
Upande wa AJTC, waliingia fainali baada ya kuichapa timu ya Taswa
Arusha, 1-0 na baadaye waliwatoa Sunrise radio kwa penati 11-12 baada ya
timu hizo kutoka sale.
Katika
mchezo wa fainali ya mpira wa pete uliochezwa uwanja wa general Tyre
jijini Arusha, Taswa Queen iliicharaza Taswa Arusha 45-0 katika mchezo
wa nusu fainali na kuisambaratisha AJTC ambao walikuwa mabingwa watetezi
kwa mabao 53-1 katika mchezo wa fainali.
Kutokana
na ushindi huo, Taswa Queen walikabidhiwa kikombe na Meneja mauzo wa
kampuni ya Megatrade, Gudluck Kway na fedha taslimu 150,000.
Katika
soka Taswa Dar pia ilifanikiwa kuingia fainali na timu ya AJTC na licha
ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kutofungana,
mshindi alishindwa kupatikana kutokana na kiza uwanjani.
Katika
michezo mingine, timu ya ORS kutoka Manyara, ilifungwa na Sunrise 2-1
na baadaye ORS iliwafungua TBL Arusha goli 1-0 na hivyo kutwaa zawadi ya
timu yenye nidhamu.
Katika tamasha hilo, katika mchezo wa kuku, wanahabari kutoka Taswa SC, AJTC na Taswa Arusha walitamba na kushinda.
Mwenyekiti
wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo
huku akiwapongeza wadhamini wao, Delina Group of Companies, Said Salim
Bakhresa & Co Ltd (Azam), DRFA na Kassim Dewji.
Tamasha
hilo la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, liliandaliwa na TASWA
Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique na kudhaminiwa na
TBL,TANAPA, Megatrade,AICC,Cocacola, Pepsi na Wazee Klabu.
0 comments:
Post a Comment