Na Mwandishi wetu
TIMU
ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) kesho
(Ijumaa) itacheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya timu ya kombaini ya
Shirikisho la Kandanda la Tanzania (TFF) na Chama cha soka cha mkoa wa
Dar es salaam (DRFA).
Mchezo
huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume na TFF itaongozwa na Katibu wake mkuu, Angetile Osiah, Boniface
Wambura (Msemaji), Saad Kawemba, Sabri na kipa, mzee Mshangama.
Mbali
ya wachezaji timu hiyo itakuwa na viongozi wengine wa DRFA akiwemo,
Msanifu Kondo, Almasi Kasongo, Mohamed Mharizo. Pia kocha mkuu wa timu
ya Taifa, Kim Poulsen, kocha wa timu za vijana, Jacob Michelsen na
wasaidizi wao kama Jamhuri Kihwelu, Peter Manyika na wengineo watakuwepo
uwanjani.
Mwenyekiti
wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa mbali ya yeye kuongoza jahazi la
timu yake, pia watakuwepo wachezaji wengine kama Ali Mkogwe, Juma
Pinto, Wilbert Molandi, Sultan Sikilo, Salum Jaba, Deogratius “Super
Deo” Maganga, Kelvin Kiwia, Julius Kihampa, Sweetbert Lukonge, Elius
Kambili, Zahoro Mlanzi, Frank Balile, Mwarami Seif, Saidi Seif na
wengine wengi.
“Huu
ni mchezo wa kudumisha ushirikiano wetu kwani sisi ni waandishi wa
habari za michezo na wao ni miongoni mwa wadau wetu, hivyo nawaomba
wachezaji wote wafike kwa wingi ili kuona mechi hiyo ya aina yake,”
alisema Majuto.
0 comments:
Post a Comment