Mshauri
wa masuala ya jinsia na mwanaharakati wa haki za binadamu, Gemma
Akilimali akisisitiza jambo katika warsha ya wahariri iliyoandaliwa na
TAMWA.
Mshauri
wa masuala ya jinsia na mwanaharakati wa haki za binadamu, Gemma
Akilimali akisisitiza jambo katika warsha ya wahariri iliyoandaliwa na
TAMWA
Sehemu ya wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini wakiwa katika warsha iliyoandaliwa na TAMWA
……………………………………………………..
CHAMA
cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimetaja mambo ya msingi ya
kuzingatiwa katika mchakato wa Katiba Mpya ili ujio wa katiba hiyo uweze
kutokomeza mila kandamizi na vitendo vya kikatili kwa wanawake.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na mshauri wa masuala ya jinsia
na mwanaharakati wa haki za binadamu, Gemma Akilimali alipokuwa akitoa
mada katika kikao cha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini
kilichofanyika makao makuu ya TAMWA Sinza.
Akizungumza,
alisema vyombo vya habari havina budi kusimama kidete na kuhakikisha
fursa ya ujio wa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa inaweza kuondoa
vikwazo na mazingira ambayo yalikuwa kandamizi kwa wanawake.
“Tunataka
katiba Mpya ibatilishe sheria ambazo bado ni kandamizi; iendelee
kubatilisha sheria zote za ubaguzi wa jinsia, ikiwa ni pamoja na
kukataza mwendelezo wa tabia, taratibu na mila zenye kubagua na
kudhalilisha wanawake na watoto wa kike chini ya mfumo dume unaotawala
jamii zetu,” alisema Bi. Akilimali.
Akifafanua
zaidi, alisema katiba haina budi kutamka wazi kuwa elimu itolewe bila
kikomo kwa jamii hiyo huku akishauri pia ibainishe kuwa nafasi za
uongozi ziwe na haki sawa ili kuleta usawa katika makundi yote hasa
wanawake.
Aidha
alisema katiba mpya iwajibishe serikali kutekeleza mikataba yote ya
kimataifa iliyoridhia kuhusu haki za wanawake ikiwa ni pamoja na
kuendeleza misingi inayolinda utu wa mwanamke na uwepo wa mahakama ya
kifamilia.
Mambo
mengine ambayo mwanaharakati huyo alitaka yawekwe wazi katika katiba
hiyo, ni pamoja na haki ya kunufaika na kumiliki rasilimali za nchi,
haki za uzazi salama, haki za huduma za msingi, haki za wanawake
walemavu, haki za mtoto wa kike na iwepo tume maalumu itakayo hakikisha
uzingatiaji wa haki za wanawake katika nyanja mbalimbali.
Alisema
madai yote hayo yamekuwa vikwazo kwa fursha nyingi kwa wanawake, hivyo
vyombo vya habari vinaweza kuendeleza mjadala huo wa madai ili kumsaidia
mtoto wa kike ambaye amekuwa akiminywa na mfumo uliopo kwa muda mrefu.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
0 comments:
Post a Comment